Nakupa pongezi kwa sababu huwezi kufikia kumi bila kuanza na moja mwendo wako uko kwenye njia sahihi, na mwelekeo wako ni mzuri!
Kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya CAF si jambo dogo; umefanya kazi kubwa na kufanikisha mengi. Nafasi hii inakupa nafasi ya moja kwa moja kushiriki katika vikao vya Kamati ya Utendaji ya CAF, chombo cha juu kabisa cha maamuzi ya mpira wa miguu barani Afrika. Hii ni hatua kubwa zaidi ya cheo chako cha Mwenyekiti wa Vilabu barani Afrika.
Wapo wanaokubeza, lakini ipo siku wataelewa, watake wasitake. Kufika juu kunakuletea fursa nyingi za kujifunza kuhusu uongozi kwa kukutana na viongozi wakubwa wa soka Afrika. Hatutashangaa kukuona ukipata nafasi za juu zaidi za kiuongozi ndani ya CAF.
Tunakutakia kila la heri!