Pongezi kwa hakielimu kuamua kufanya utafiti matokeo ya kidato cha nne

Pongezi kwa hakielimu kuamua kufanya utafiti matokeo ya kidato cha nne

Sungurampole

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2007
Posts
984
Reaction score
205
Nimesoma na kufarijika sana kuwa Shirika la haki elimu limeamua kufanya utafiti wa kina kwa shule ya sekondari ya Kariakoo iliyopo manispaa ya Tabora kwa lengo kubaini chanzo cha kufanya vibaya kwa shule za sekondari nchini.
Sijui kigezo walichotumia kupata shule hii na pia sijui itakuwa representative kwa kiasi gani lakini bado naamini tuna uwezekano mkubwa wa kupata yaliyojificha katika kadhia hii. Najua kuna tume ya Pinda lakini watanzania tuna kila sababu ya kutokuwa na imani na tume zinazoundwa na serikali kwani hawana record ya kuja na lolote jipya sana tunuona kama ni ulaji mwingine huku tatizo likibakia pale pale kama siyo kufukiwa.

Bravo Hakielimu songa mbele na mkiona vipi fikirieni kuongeza sample - hata ikibidi tuwachangie gharama naamini watanzania wengi nikiwa mmoja wao tutakuwa tayari kufanya hivyo

(source- Baruti 27.2.2013)
 
hiyo shule iitwayo kariakoo ipo sehemu gani ya tabora? and how old is it?
 
Katika mambo ya kupongezwa waliofanya haki Elimu ni pamoja na tafiti zao mbalimbali kuanzia mazingira ya kufundishia, umuhimu wa vitendea kazi,morali ya walimu katika kufundisha vijijini na tafiti nyngine. Jambo la ajabu ni kwa serikali kushindwa kuyatumia mapendekezo ya tafiti za haki elimu na matokeo yake ndio hayo tumeyaona ya kufeli kwa 60% ka wanafunzi. Nadhani matokeo ya utafiti wa shule ya sekondari kariakoo Tabora ni changamoto kwa watawala. Hongera haki elimu.
 
Back
Top Bottom