Pongezi kwa mabinti

xfactor

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
1,511
Reaction score
1,289
Habari zenu wadau

Ukiachilia mbali kasoro mbalimbali za matokeo ya kidato cha nne,ambazo binafsi sizishangai sana maana elimu ya sasa nchini kwetu imekuwa ni siasa.

Binafsi swala kubwa nililoliona na kunivutia ni performance ya watoto wa kike.Naomba tuchukue fursa hii kuwapongeza mabinti kwa kufanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha IV.

Sijafanya utafiti kujua matokeo kwa ujumla ila kwa kuangalia tu wanafunzi kumi bora yatosha kabisa kuwapongeza mabinti.Ile dhana potofu kuwa wanawake hawawezi au mtoto wa kiume ni bora kuliko wa kike haina nafasi tena.

Kwa upande wa pili kuna jambo pia la kujiuliza,watoto wetu wa kiume wana shida gani? Si kama ni mbaguzi wa jinsia,la hasha ila nia na dhumuni ni kuwepo na ushindani utakaoleta uwiano au pengine wakiume nao wana changamoto wanazopata hvyo tunapaswa kuzijua ili kuwasaidia.

"Mama ndio ulimwengu,elimisha mwanamke uelimishe ulimwengu"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…