Pongezi kwa Mamlaka kwa kupambana na Panya Road

Pongezi kwa Mamlaka kwa kupambana na Panya Road

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Pongezi kubwa kwa Jeshi letu la Polisi kwa kazi nzuri wanayo endelea kuifanya kuhakikisha hakuna cha panya rodi wala panya buku.

Pongezi pia kwa Mkuu wa Mkoa wa DSM Makala kwa kuweka mikakati madhubuti ya kutokomeza uhalifu katika Jiji la DSM.

Ushauri;

1. Zoezi la kupambana na uhalifu haswa kwa Mkoa wa Dsm liwe endelevu ma nguvu hiyohiyo.

2. Doria ya mara kwa mara inasaidia sana, sio hadi tukio ndio Polisi wafike eneo husika.

3. Vijiwe vya uvutaji bangi visafishwe na viteketezwe maana hivyo ndivyo mazalia ya uhalifu.

4. Kila taarifa ya uhalifu ifanyiwe kazi kwa uhakika bila kupuuzia.

5. Wananchi wema washirikishwe kikamilifu katika kutoa taarifa za wahalifu.

6. Wanunuzi wa mali za wizi nao wabainishwe na wakamatwe.

Ushauri kwa Panya rodi.

1. Uhalifu haulipi zaidi ya kifo
Fanyeni kazi halali hauto sumbuliwa na Jeshi la Polisi
 
Hio solution ya mda mfupi. Tutafute ya mda mrefu nini kifanyike kuzuia panya
 
Nimeona kaujumbe huko tweeter "Chizi anachekesha akiwa hatoki katika familia yako." Humo ndani kuna panya road ambao ni wa kudhan pia ila askari wameamua kkjichukulia sheria mkonon, wao wanaua tu
 
Nimeona kaujumbe huko tweeter "Chizi anachekesha akiwa hatoki katika familia yako." Humo ndani kuna panya road ambao ni wa kudhan pia ila askari wameamua kkjichukulia sheria mkonon, wao wanaua tu
Waue tu, tena waongeze spidi. Kama wewe unahisi unaweza kudhaniwa ni panya road jisalimishe! Utakula shaba.
 
Nimeona kaujumbe huko tweeter "Chizi anachekesha akiwa hatoki katika familia yako." Humo ndani kuna panya road ambao ni wa kudhan pia ila askari wameamua kkjichukulia sheria mkonon, wao wanaua tu
Watapoa baadaye watarudi tena
Ndio maana kuna umuhimu wa kuwapeleka kuzimu hawa madogo, wengi walishatumikia vifungo, hawastahili tena kupelekwa gerezani.
 
Back
Top Bottom