http://issamichuzi.blogspot.com/2008/02/pongezi-toka-india.html#comments
PONGEZI KWA MH RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE
Napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza rais wetu Mh Kikwete kuchaguliwa kwake na umoja wa Afrika kuwa mwenyeketi kwa kipindi cha mwaka mmoja,mh rais nakupongeza sana na ninakutakia kila la kheri katika kazi hii nyeti .pili nakupongeza kwa hotuba yako nzuri ya mwisho wa mwezi wa kwanza(january) mh ,hotuba yako ni ndefu na nzuri sana na ziara yako ya mkoa wa kagera.
Nikianza na hili la umoja wa afrika ,hili litasaidia katika kuitangaza nchi yetu ya Tanzania kisiasa ,kiuchumi na kijamii,kwani naamini kabisa katika safari zote za kikazi mh rais atakuwa akitumia kofia zote mbili katika kuitangaza afrika na Tanzania kiujumla. Afrika imefika mahali ambapo inahitaji kuwa na misingi mizuri ambayo itasaidia nchi zake kujikwamua kiuchumi,kisiasana kijamii ,misingi hiyo ndio imesaidia jumuiya kama za asia(India,Srilanka,maldives,pakistan),asia ya kati kama Thailand,Singapore,Malyasia,Indonesaia nk ,jumuiya hizi zimefikia mahali ambapo nchi za kibepari zimekuwa hazi lali usingizi kutokana na maendeleo yake yanayopatikana kila kukicha,
Leo, London stock exchange inajiuliza what happen at Mumbai stock exchange to day?,zamani ikiitwa Bombay,(India) shangai,hongkong,tunahitaji nasi tufike mahali wajiuleze what happen at Dsalaam,Cairo,Lagos,Johanesburg, ?na nk,tukiweza kufika hapo basi yale yote wanayofikiri kuhusu Afrika yatakuwa yakiwasuta wao wenyewe kama yanavyowasuta yale yanayotokea Mumbai,Hongkong,,Bangkok na nk
Pili nakupongeza Mh rais ktk hotuba yako ya mwisho wa mwezi wa kwanza(january),ktk hotuba yako jambo la mwisho ndilo ambalo naamini limewavutia wengi na mimi binafsi,kuhusu maadili ya viongozi na uongozi ,hili ni jambo kubwa sana katika kuhakikisha nchi inasonga mbele, ni lazima ;wala si hiari kwa wale wote wanaopenda kutumikia uma wa nchi zao kuachana na biashara ya aina yeyote kama wanazo ,hili litasaidia kupunguza rushwa ,umimi,usisi,uwao katika maslahi ya Taifa,Mh rais naamini hii ni ishara kwamba what next after that
.,na kwa kuwa limejadiliwa na kamati kuu ya CCM,litafika serikalini muda si mrefu na kupelekwa bungeni kama muswada,ili lipitishwe kuwa sheria,mh rais nakuombea kwa mwenyezi mungu maisha marefu,afya njema ili uweze kulisimamia hili kwa uadilifu,nchi kama India zaidi ya hili haihitaji raisi,waziri mkuu,mbunge,waziri kiongozi,katibu mkuu na nk kuwa na nyadhifa mbili zaidi ya ile moja aliyokuwa nayo(hili lipo katika katiba yao)tunafaham katiba ya India ndio kubwa kuliko zote duniani,nchi za kibepari katiba zao zinaingia kwa India ..,kama ifuatavyo
.marekani mara saba,France mara tano,Australia mara sita na nk
Katika hili la maadili ya viongozi na uongozi, ndio linalotokea leo hii kwa mfanyabiashara maarufu na mmliki wa manchester city ya uingereza(football club) Dr Thaksin shinawatra alipokuwa waziri mkuu wa Thailand siku za nyuma ,leo hii ana kesi ya kuhusiana na rushwa alipokuwa waziri mkuu,japo alikuwa ni mfanyabiashara hata kabla hajawa waziri mkuu wa Thailand.
Nampongeza Mh raisi pia katika ziara yake ile ya mkoa ule wa kagera ,pale alipozungumza na wananchi wa muleba/Biharamuro na kusisitiza katika suala lile la ujambazi ,kwa kuwataka wanaowafaham majambazi hayo wayataje ,ama yajisalimishe yenyewe,ni kweli wananchi wanawafaham,kwani ni wajomba,mtoto wa kaka,dada,binamu,nakuunga mkono 100% kuweka mikakati mipya ambayo itasidia kulikomesha hili,ambalo limekuwa sugu sana kwa sasa,wenzetu wanasheria inayosema shoot order to kill hii ikiwa na maana ukihisiwa tu kuwa wewe ni jambazi basi unauwawa,hakuna mahakamani wala gerezani nchi kama Brazil,Nigeria,Amerika ,Afrika ya kusini hili linafanyika na nchi nyingine nyingi tu duniani , hata jirani zetu Kenya ilikuwepo wakati wa utawala wa Moi miaka fulani fulani, sijui kama bado iko au la...,lakini mm nasema iliwasaidia jirani zetu naamini kwa Tanzania tunahitaji mbadala wa hili ,ambalo litawezesha kumaliza suala la ujambazi nchini.
Napenda kumtakia Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete afya njema,maisha marefu na vilevile naitaki a nchi yangu ya Jamuhuri ya muungano waTanzaia amani na upendo na afrika kwa ujumla.