Pongezi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete

Pyaar

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2018
Posts
16,078
Reaction score
77,186
Huduma za afya kwa hospitali za Umma mara nyingi zimekuwa zikilalamikiwa na jamii kuanzia matibabu mpaka lugha kwa wagonjwa, lakini utofauti mkubwa umeonekana Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Pongezi nyingi kwa Mkurugenzi na Madaktari wote bila kusahau dawati la huduma kwa wateja (Customer Care Desks).

Mnaitendea haki JKCI.

👑👑👑👑👑👑👑👑
 
Ilipoanzishwa iliwekwa misingi mizuri sana.

Engineer Kikwete, Chief Technician Janabi.

Main Financier Prince Walid bin Talal.

Donor: Bill Gates.

Kuna kukosewa msingi hapo?
 
Hamna hospitali hapo ndiyo maana rais,makamu waziri mkuu akiugua hawezi kupelekwa hapo zaidi atapelekwa India au ulaya.kama umetembelea Nchi nyingi utagundua hapo hamna kitu
 
Kuna vitoto vinambeza Prof. Hua naangalia nasema legacy yake katika Taifa ni kubwa ndio maana kila Rais hataki kumwachia

Alitajwa kuwapo kwenye ile timu kabambe wakati jiwe akiomba kurejeshwa nyumbani.

Au nasema uongo ndugu yangu?
 
Huduma za afya kwa hospitali za Umma mara nyingi zimekuwa zikilalamikiwa na jamii kuanzia matibabu mpaka lugha kwa wagonjwa, lakini utofauti mkubwa umeonekana Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Pongezi nyingi kwa Mkurugenzi na Madaktari wote bila kusahau dawati la huduma kwa wateja (Customer Care Desks).

Mnaitendea haki JKCI.

👑👑👑👑👑👑👑👑
Siku hzi tunao madaktari ambao unaweza ukafikiri ni Malaika wameshushwa kutoka Mbinguni; kwa kazi na kwa maadili pia
 
Ni sahihi kabisa.
Ila hii nimeiona JKCI pekee, kwingineko hata uzubae zubae koridoni hakuna wa kukushtua.
 
K
Ilipoanzishwa iliwekwa misingi mizuri sana.

Engineer Kikwete, Chief Technician Janabi.

Main Financier Prince Walid bin Talal.

Donor: Bill Gates.

Kuna kukosewa msingi hapo?
Kwakweli hawabahatishi.
 
Siku hzi tunao madaktari ambao unaweza ukafikiri ni Malaika wameshushwa kutoka Mbinguni; kwa kazi na kwa maadili pia
Mkuu, huduma nzuri sio guarantee ya kutokupoteza uhai, madaktari wanapambana kwa kiasi chao lakini inapotokea jitihada zao kugonga mwamba wanakuwa hawana namna.
 
Hiyo haimanishi ulichotendewa wewe au kuhudumiwa ndivyo na wengine wanapata huduma hiyo,lah! Pia itategemea na watoa huduma wa wakati huo. Maboresho katika huduma ya afya yanahitaji KWa kiwango kikubwa maana bado tunajikongoja KWa hatua.
 
Hamna hospitali hapo ndiyo maana rais,makamu waziri mkuu akiugua hawezi kupelekwa hapo zaidi atapelekwa India au ulaya.kama umetembelea Nchi nyingi utagundua hapo hamna kitu
Mkuu, tumelinganisha na hospitali zetu za UMMA tulizonazo.
 
Back
Top Bottom