Hivi unafikiri kuna mmachinga atakae unga mkono kwa huo upupu wenu wa kutaka elf 10000? unafikiri kuna mkulima aliyeko kule mbinga atasikiliza ujinga wenu? kwanza watashangaa kwamba hata kuna watu wanapata 5000 kwa siku. Ninachowashauri ni kwamba ili mgomo wenu uwe na mashiko lazima muwe na ajenda kuu zenye misingi ya kudai mabadiliko ya mfumo ambayo eventually yataleta sustainable changes.
Nikuulize, hivi leo mkipewa 10000, halafu inflation ikaendelea kama ilivyo mpaka kufikia 30% unafikiri hiyo elfu 10 itatosha? Nasikitika kwamba hata nyie tunaowaita wasomi ni bure kabisa, bora serikali ingetumia nguvu kuwapeleka wote veta na vyuo vingine vya ufundi ili baadae tupate watu wanaoweza kuzalisha tangible products kuliko kuwa na maelfu ya watu wanaosomea ualimu wa historia, civics na geography huku wakitaka waongezewe boom mpaka elf 10000.
Hivi wewe unajua kuwa kuna watu wengi tu wasiopata hiyo 150,000 (5000*30) kwa mwezi? Hoja zenu nyepesi na ni kero kwa watu wenye akili timamu wanaodai mabadiliko ya kweli. Kwa nini msiandamane kupinga malipo ya dowans? kwa nini msiandamane kudai katiba mpya? kwanini msiandamane kupinga kutochukuliwa hatua za maana kwa mafisadi papa? kwa nini msiandamane kupinga mfumuko wa bei (ambao hautaisha kwa nyinyi kupewa 10000/day), kwa nini msiandamane kuwa kwenye vyuo vikuu visivyokuwa na facilities za kutosha kama vitabu na computers?.
Tatizo lenu wengi mmesoma elimu za kwenye majarida ya msabila na nyambari nyangwine na hapo chuo kikuu mkishasoma slides za walimu basi huna habari na vitabu (hata vikiwepo). Kwa kifupi taifa hili halina tena vyuo vyenye kuzalisha wasomi ila tuna taasisi za kusaidia vijana wakue huku wakijidanganya wanasoma.
Serikali embu pelekeni veta hawa wahuni wanaofikiria matumbo yao (eti 10000/day) bila kuangalia hali halisi.
NB: Pale kwenye bluu nadhani ulitaka kuandika FIKIRIA lakini kwasababu ya elimu za kudesa hata spelling check ni tatizo kwako.