Pongezi kwa Zakazakazi kuufafanua mgogoro wa Israel na Palestina kwa facts na kuweka udini pembeni

Wakatoliki wa Peramiho ni Watanzania, Wayahudi sio Wapalestina au Waarabu.
Nchi ya Israel imekuwepo karne na karne katika Historia.
Weka ushahidi wa uwepo wa Israel kabla ya mwaka 1948.
 
walikuwa wakimbizi kutoka wapi, hyo nchi waliyokimbia inaitwaje au ilikuwa inaitwaje?
 
Wakatoliki wa Peramiho ni Watanzania, Wayahudi sio Wapalestina au Waarabu.
Nchi ya Israel imekuwepo karne na karne katika Historia.
Siyo wote, wengi wa mwanzo walikuwa ni Wazulu (Wangoni) wa kutokea Afrika Kusini, waliletwa na Wajerumani kupigana vita ya majimaji.
 
Hivi wakatoliki wa peramiho leo hii wakisema wanaanzisha nchi yao hapo peramiho kwa kuwa wapo 100% wakatoliki na eneo hilo walipewa na Wajerumani walipokuwa wanatawala kimabavu basi ndiyo imeshakuwa sawa hivyo?
Mfano irrelevant, tunataka kujua origin ya hawa wayahudi unaosema walipewa hifadhi hapo palestina na wapalestina. walitoka wapi, ebu tuanzie hapo.
 
Siyo wote, wengi wa mwanzo walikuwa ni Wazulu (Wangoni) wa kutokea Afrika Kusini, waliletwa na Wajerumani kupigana vita ya majimaji.
Rekebisha mfano wako sasa useme Wangoni wakitaka kujitenga na kuwa na taifa lao, kwa sababu Wangoni wengine ni Waislamu, Wapentekoste, Walutheri, Wapagani n.k Sio sahihi kuwachukulia Wangoni wote Wakatoliki.
 
Ki ufasaha unatakiwa uandike wakristo. Siyo wakristu. Pia ni Yesu Kristo na siyo Yesu Ktistu.
Sisi Catholics tunaita hivyo 'Wakristu' na 'Yesu Kristu' na ndivyo tumezoea lakini sioni shida kwa anaeita 'kristo'
 
Rekebisha mfano wako sasa useme Wangoni wakitaka kujitenga na kuwa na taifa lao, kwa sababu Wangoni wengine ni Waislamu, Wapentekoste, Walutheri, Wapagani n.k Sio sahihi kuwachukulia Wangoni wote Wakatoliki.
Hapana, sivyo utakavyo wewe, haiendi hivyo.

Wewe unaweza weka post au uzi wako upendavyo.
 
Asante sana,hapa nimeongeza maarifa
 
Weka ushahidi wa uwepo wa Israel kabla ya mwaka 1948.
Nenda Israel kahiji, wataanza kukutembeza kuanzia Western/Wailing Wall. Kwa msaada zaidi unaweza kumtafuta Job Ndugai akuelekeze. Vitabu vya Historia anza kusoma Israel and the Nations; F.F Bruce, David F Payne.
 
Hiyo ardhi awali ilikaliwa (kwanza) na Wafilisti kaka, kabla Joshua hajaamuriwa awasngamize wenyeji wote ili Israel akae.

Tukiongea uongo hata haisaidii ukristo wetu
..."kabla Joshua hajaamuriwa awaangamize wenyeji (Palestines)wote ili"...
 
Hii mistari yako haisaidii chochote, guys we want to know the origin of jews kabla hawajaenda kuvamia hzo nchi za watu kama mnavosema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…