MWANGAKE ANTHON
Member
- Nov 30, 2013
- 5
- 3
Awali ya yote napenda nitumie nafasi hii kukupongeza kwa ushindi wa jana,wewe ndiye MWENYEKITI mteule wa BUNGE la KATIBA.
Katika hoja zako, ukiwa unajinadi ulisema maneno mawili
1."mkinipa kura mimi sawa na kumrusha chura kwenye dimbwi" FASILI yake wewe umelizoe bunge na kazi yake, TAFADHARI mzee usije fanya kazi kwa mazoea pekee, hili ni bunge la kuipeleka nchi zaidi ya miaka 30 TOFAUTI na bunge la BAJETI inayoisha ndani ya mwaka mmoja.
2."Watakao pinga muungano nitawashughulikia", FASILI yake wewe ni muumini wa muungano hivyo kati ya mambo yote wewe kama mwenyekiti, pia utafanya kazi ya kulinda MUUNGANO.Hii si vema, wewe kama mwenyekiti naomba wanaoelezea hisia zao juu ya MUUNGANO washindwe kwa hoja wala si kwa kukosa ushirikiano toka kwako kama mwenyekiti wao.Je hao watu 69 waliompigia kura Hashimu Rungwe unadhani ndiyo wasiopenda baadhi ya taratibu za MUUNGANO? La hasha , walio kupigia kura wamekupigiakura bila kujali wewe ni wa chama gani, una mtazamo gani juu ya katiba, HIVYO kwa kutambua weredi wako kama ilivyo kuwa kwenye bunge enzi zako.
OMBI/USHAURI
Mhe Samwel Sitta, watanzania wafuatao wanakutegemea wewe
1.Wenye ulemavu
2.Wanasiasa(vyama vyote)
3.Wasio na chama cha siasa
4.Wakulima
5.Wafanyakazi
6.Wavuvi nk
Natambua kuwa wewe ni mwana CCM tena kiongozi mwandamizi, lakini mzee wangu enzi za bunge uliloliongoza haukuwa na tatizo kwa maana ya kuegemea katika chama.Tambua kuwa watu walio kupigia kura si CCM pekee,bali CUF, NCCR MAGEUZA, TLP,UDP,CHADEMA nk wamekupigia kura kwa kujenga imani nawe kutokana na uzoefuwao juu yako
PIA,Natambua kuwa ndani ya CCM, lazima upewe HADIDU ZA REJEA toka kwa mabosi wako kichama.Tambua kuwa hakuna hata BOSS mmoja wa CCM alaliyekupigia kampeni, bali UZALENDO WAKO, UCHAPAKAZI WAKO NA UPENDO WAKO kwa wanyonge ndiyochachu ya ushindi.
Haujapata hiyo nafasi kwakuwa wewe ni mwanaCCM, kwakuwa wewe ni WAZIRI, kwa kuwa wewe si CUF,CHADEMA,NCCR nk bali IMANI YA WATANZANIA juu yako ndiyo siri ya MAFANIKIO YAKO
Nakuomba mzee Sitta,
1.Usije ogopa kukubali matakwa mazuri yenye tija kwa taifa ya CCM eti utasemwa unapendelea
2.Usije kataa matakwa mazuri na yenye tija kwa taifa toka vyama vya upinzani,kwa kuwa wao ni vyama tofauti au kwa kuogopa ndani ya chama chako utasewa umekiuka makubaliano
3.Usije ongoza kwa kutaka unachokitaka kifanikiwe, bali ongoza kwa utashi na kuheshimu mawazo ya watu.
MUNGU AKUBARIKI, KAZI NJEMA