Eng. Zezudu
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 8,024
- 11,546
Ila hapa roho inakuuma kwemba kweli unamuunga mkono Gwaji boy.Kiukweli kabisa, nilitaka kusema, Magufuli akipewa kipindi cha pili, ataumaliza kabisa umasikini, naomba kurekebisha, nikisema akipewa ni kama nimeonyesha kuna possibility asipewe, wakati hali halisi ni JPM, ameishashinda zamani, kinachotafutwa sasa ni kura nyingi tuu za kutosha!. Hapo alipo tayari anayo over 80% victory, tunahangaikia ipande hadi 90%, na wiki ya lala salama, tufike over 95%.
Kwa maendeleo ya Tanzania,
Chagua Magufuli,
Chagua CCM,
na kwa jimbo langu la KAWE, Twende na GwajiBoy!.
P
Nenda ukapige kura yako.Wanabodi,
Na kwa vile ni mwaka wa uchaguzi mkuu, kuna wanasiasa ambao watapanda jukwaani na kujinadi kuwamkituchagua tutafanya hiki na hiki na hiki, lakini kuna wengine, watapanda jukwaani sio tuu kusema, bali kuonyesha walichofanya, hivyo naomba kuwaandaa watu kisaikolojia, usije kufika muda huo, watu ambao hawana chochote cha kuonyesha kuwa wamefanya, watakapo takiwa kupanda kilingeni na watu wenye good track records za waliyoyafanya, kisha wasio na kitu wakaamua kuweka tena mpira kwapani, nashauri tuu, lets save time, money and resources, kama Watanzania tunachotaka ni maendeleo, na maendeleo hayo yanapatikana, yanaonekanika, then kwa nini tusiwaache tuu tuendelee tuu bila kufanya ....
naomba nisimalizie watu wasije kuniparura bure humu.
P
Wanabodi, mimi ni miongoni mwa wana jf, tuliandika mengi kumhusu rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo kipindi hiki cha maombolezo, napitia baadhi ya mabandiko kwa ajili ya kumuaga rasmi.Wanabodi,
Hili ni bandiko la pongezi kwa Rais Magufuli na awamu yake ya tano..
Leo nilikuwa napitia ripoti ya Benki ya Dunia(WB) kuhusu hatua ambazo zimechukuliwa na nchi mbalimbali kupunguza umasikini uliotopea, I was surprised kukuta Tanzania ndio nchi ya kwanza inayoongoza duniani kwa kupiga hatua kubwa zaidi kuondoa umasikini uliotopea, hivyo japo data ni miaka iliyopita, lakini ripoti ni mwaka huu!, hapa tunajadili ripoti ya 2019 na sio data ni za lini, hivyo Rais Magufuli na serikali yake ya Awamu ya Tano, wanastahili pongezi za dhati kwa kufanya maajabu makubwa kabisa katika vita dhidi ya umasikini uliotopea kwa kupiga hatua kubwa zaidi kupunguza idadi ya familia zilizokuwa zinaishi chini ya kipato cha dola moja kwa siku.
P