Pongezi sana kwa Dodoma Jiji Fc, ndio wamepanda daraja na wamefanya vyema katika TPL

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
44,855
Reaction score
189,385
Habari.

Nimetazama takwimu zilizotolewa na TFF juu ya mapato yaliyokusanywa na vilabu vyote kwa msimu 2020/2021.

Ukiachana na Dar Young Africans ambao wameongoza kwa mapato ya 986.8Ml kwa mashabiki 141,681. Huku Simba SC akifatia kwa mapato ya 929.7Ml kwa mashabiki 138,518.

Namba tatu amekuwa Dodoma Jiji Fc ambaye ndio msimu wake wa kwanza wa Tanzania Premier League.

Dodoma Jiji Fc anawapa taarifa clubs zingine zimebweteka na kushiriki kwa mazoea.

Dodoma Jiji Fc hadi anamaliza league alikuwa na msimu bora pia japo ndio alikuwa amepanda daraja.

Napenda kuwapongeza uongozi na mashabiki wa Dodoma Jiji Fc waliojitokeza kwa timu yao changa ila imefanya vyema kabisa.

Dodoma Jiji Fc ameingiza mapato ya Sh 148.1Ml akiwa ameshika nafasi ya tatu kwa ukusanyaji wa mapato.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Kongole Dodoma Jiji FC.

Cc: Kichwa Kichafu
 
Hio dodoma jiji imeingiza mashabiki wengi nyumbani na kupata pesa nyingi nyumbani kupitia mechi mbili tu ambazo ni simba na yanga
Jiulize kwanini Dodoma Jiji?

Maana hata hao wengine pia wamecheza mechi hizo hizo( Young Africans & Simba SC)

Mtazame Azam, Namungo, KMC, Kagera, Mtibwa na wengine wote.


Kongole Dodoma Jiji Fc!
 
Hio dodoma jiji imeingiza mashabiki wengi nyumbani na kupata pesa nyingi nyumbani kupitia mechi mbili tu ambazo ni simba na yanga
Kwanini Azam hakupata hizo pesa kupitia mechi hizo mbili?
 
Hiyo ni kwa sababu timu imepanda daraja
Hata Lipuli ilikuwa hivi
 
Ingekuwa kipindi kile hizi pongezi zingesindizwa na yale maneno ya awamu ya 5
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…