Pongezi za watendaji wa kata Tanzania kwa Rais Samia

Pongezi za watendaji wa kata Tanzania kwa Rais Samia

AUGUSTINO CHIWINGA

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2017
Posts
220
Reaction score
689
Tunakusalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kazi iendelee!

Awali ya yote tunapenda kuchukua fursa hii kukutakia heri na fanaka katika mwaka mpya wa 2023. Pia tunakupongeza kwa juhudi zako mbalimbali za kuliletea maendeleo Taifa.

Mh. Rais sisi watumishi wako katika kada ya Watendaji wa Kata tutakua wachoyo wa fadhila endapo tutashindwa kukushuru wewe binafsi na Serikali yako kwa namna ambavyo umetuheshimisha na kututatulia changamoto zetu za muda mrefu zilizokua kero katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kiutumishi wa umma.

Tangu uingie madarakani tumeiona dhamira yako njema kwetu, kwani tumepata stahiki zetu za kisheria kama watumishi wa umma, kama vile nyongeza ya mishahara na kupanda madaraja.

Lakini kipekee kabisa ni uamuzi wako wa kukubali na kupitisha Watendaji wote wa Kata nchi nzima wawe wanapata posho ya madaraka kila mwezi

Mh. Rais posho hiyo imekua ni msaada mkubwa kwetu katika kutekeleza majukumu ya kiserikali , kwani hapo awali hali ilikua ni mbaya sana.

Pia tunashukuru kwa uamuzi wako wa kukubali na kupitisha ununuzi wa pikipiki kwa ajili kurahisisha usafiri kwetu Watendaji wa Kata nchi nzima, Tatizo la usafiri lilikua ni mojawapo ya kikwazo kikubwa katika utekelezaji na ufuatiliaji wa majukumu yetu ya kila siku kwa hatua hiyo sio kikwazo tena.

Mh.Rais kama inavyojulikana kwamba Mtendaji wa Kata ni kiungo muhimu katika utekelezaji wa shughuli zote za Serikali katika Kata yake lakini kwa kipindi kirefu kada hii iliachwa nyuma tofauti na wewe Rais wetu ambaye kwa vitendo umeonesha kuitambua ,kuijali na kuithamini kwa kiasi kikubwa na ndio maana umeamua kuifanyia mema na maboresho makubwa sana kama hayo tuliyotangulia kuyasema hapo juu.

Tunakuomba Mh.Rais uzidi kuingalia kada hii kwa jicho la tatu uzidi kuiboresha na kutatua changamoto zetu zilizosalia, ambazo endapo tutapata nafasi tutaziwasilisha kupitia kwa Waziri wa TAMISEM Mh. Angellah Kairuki.

Ahadi yetu kwako ni kwamba tutaitekeleza Ilani ya Chama vizuri katika Kata zetu.
Tutazidi kuwa watiifu kwa Serikali na kuyaeneza yote mazuri ambayo Serikali yako makini ya Awamu ya Sita inayoongozwa nawe inayatenda nchi nzima kupitia miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambayo inatekelezwa katika Kata zetu na kusimamiwa kwa karibu na sisi Watendaji wa Kata.

Tutakuwa nawe bega kwa bega katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

Imetolewa na;
Augustino Chiwinga

Mwenyekiti wa Kamati ya kuunda umoja wa Watendaji Tanzania.
24/01/2023
 
Zile 5000 za muhuri mhe.rais anazitambuaga?
 
Back
Top Bottom