Pongezi: Zanzibar inaenda vizuri kwenye utalii

Pongezi: Zanzibar inaenda vizuri kwenye utalii

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Kwa miaka yote nilikuwa nikitaka kwenda Tanzania kwa KLM ilikuwa lazima ipitie KIA kushusha wageni lakini kwa mara ya kwanza ndege yangu itatua Zanzibar halafu inaenda Dar.

KLM siku moja wanaenda Zanzibar na siku inayofuata wanaenda KIA. Lakini hoteli za Zanzibar nimeona zimepanda bei sana kwa maana watalii wameongezeka sana.

Hizi ni kati ya zile pongezi ambazo ni lazima tuzitoe. Tuhakikishe tu mapato yanatumika vizuri na hizo hotel wasije wakawa na account nje halafu pesa ziwe zinabaki huko nyingi.
 
Naona mnapingana, yule anachafua wewe unasafisha, binafsi sijawahi kuelewa CCM inatupeleka wapi kama taifa.
 
Back
Top Bottom