Mkuu kwanza naomba uelewe kuwa mtoto anatokana na genes za wazazi, kama wazazi micharuko ni ya kurithi basi mtoto hata umlelee mbinguni atasala tu.Pili mtoto anazaliwa akiwa na akili tupu(tabolarasa),hivyo ni jukumu lako wewe mzazi kuijaza akili hiyo kile ambacho ni sahihi kwa maisha ya mwanadamu.
Kama utaijaza akili hiyo ugomvi,matukano,uzinzi,na yote yasiyofaa basi kwa vyovyote vile mtoto huyo atakuwa asiyefaa hata umlelee whitehouse.Tatu mtoto anaharibiwa na mazingira anayoishi pamoja na watu anaokutana nao,hivyo ni jukumu lako kama mzazi kujenga ukaribu na mtoto wako ikiwa ni pamoja na kujua muda wote yuko wapi na anafanya nini na sio wewe mzazi kuwa kama simba,watoto wakikusikia umerudi tu wao mbio kujifungia au kutoka nje ili kukukwepa.
Na unapokuwa karibu na mtoto jitahidi kuelewa ameitumia vipi siku yake na unapoona amekosea jaribu kumrekebisha mapema kwa upendo na upole na si kumrukia kwa makofi na bakora hata kwenye yale ya kuelezana tu.Hivyo basi kwa upande wangu naona sehemu yoyote haina tofauti katika malezi ya mtoto hasa kama unapokuwa makini katika kuwajenga na kuwatunza wanafamilia yako kama ukizingatia hayo niliyo kuambia hapo juu.Dar ni sehemu tu kama zilivyo nyingine kuna wanaoharibikiwa na wanofanikiwa.
Mimi nimezaliwa Dar keko magurumbasi,nimekulia sinza miaka 20 baada ya hapo wazazi wakawa wameshahama sinza na kwenda mbezi beach(yote hiyo ni dar).Mimi nimeweza kuondoka dar na kwenda mikoani ambako niliweza kufanya kazi mpaka nilipopata nafasi ya kufanya kazi nje ya nchi.Sasa hapo ubaya wa dar uko wapi.Kikubwa nachoweza kuwashauri vijana wenzangu ni kuwa makini wakati unapotaka kuwa na mwenzi wa maisha.
Sio unaona kidada kimepaka wanja nakupendeza basi unachanganyikiwa bila kujua tabia zake na ukoo wake.Mwisho wa siku utakuja leta viumbe wasioeleweka humu duniani na kuanza kuilaumu Dar es salaam yetu bila kukumbuka kuwa kila sehemu dunia hii ina wema na wabaya.