BL, Exaud etc,
Kilam mmoja wenu anaweza kuwa sahihi kwa namna moja au nyingine!
Kwanza kabisa naomba kabla ya kuchangia hii kitu, tutofautishe aina za kodi hapa, then kwa kila moja tuangalie kundi lipi (matajiri na masikini or walaji wa mwisho) ambalo huchangia zaidi kodi kwa taifa.
Kuna makundi makubwa mawili ya kodi nayo ni;
a) Direct taxes
b) Indirect taxes
Direct taxes ni kodi ambazo burden yake hubebwa moja kwa moja na mtu anaye lipa kodi husika. Mfano wa kodi hizo ni kama, kodi ya makampuni (corporate tax), kodi za zuio (withholding taxes), kodi zitokanazo na ajira (employment taxes e.g PAYE AS YOU EARN -PAYE), kodi kutoka kwenye investments etc. Kwa aina hizi za kodi, kadiri mtu anavyopata kipato kikubwa ndivyo anavyo changia kodi kubwa zaidi, kwa kuwa zote ziko based on asilimia fulani ya pato lako au faida yako. Hivyo, ukiangalia aina hii ya kodi watu wa kipato cha juu, wanalipa zaidi ya wale wa kipato cha chini...Mfano, katika sheria ya kodi ya mapato Mwaka 2004, (ITA 2004), kama wewe umeajiriwa na unapata mshahara pamoja na marupurupu mengine yasiyo zidi Tshs 100,000...hutakiwi kulipa kodi kabisa, wakati wanaopata kiwangu kikubwa zaidi ha hiki, hutakiwa kulipa kodi, ingawa nao wanasamehewa laki moja ya kwanza! au kama unakodisha nyumba unatakiwa kulipa 10% ya rent kama kodi ya zuio, hivyo kadiri mtu anavyopata rental income kubwa ndivyo atakavyochangia zaidi!
Indirect taxes hizi ni kodi ambazo burden yake humpata mlaji wa mwisho.....sasa hapa mlaji wa mwisho si lazima awe masikini! mfano wa kodi hizi ni kama, VAT, Stamp duty, exercise duty, import duty etc. Sasa tuchukilie mfano wa mfanyabiashara (company or sole propriator) say anauza nguo ambazo kaziingiza toka nje ya nchi. Huyu bwana, akimport hutakiwa kulipa VAT (20%), Import duty (25%) etc hizo kwake anazifanya kama gharama za bidhaa (nguo) alizo agiza, so bei yake ya piece moja ya nguo itatake into account kodi hizo, kama yupo registered kwa VAT kwa mfano, atakapo uza nguo zake kwa mfano anatakiwa kucharge VAT tena ya 20% (hii si gharama yake) kwa mnunuzi wa mwisho anayeenda kuvaa nguo husika.....! mnunuzi wa mwisho hana kwa kuidamp hiyo VAT, so final consumer ndiye mlipaji halisi wa INDIRECT TAXES. Lakini, ukichukulia the fact that, wafanyabiashara kama consumers wa bidhaa na huduma mbalimbali, burden ya kodi hii nao huipata wanapo kuwa wanaincur expenses for private purposes (not for business). Hivyo, burden ya indirect tax ukilinganisha Business vs individual consumers / final consumers ndio walipa kodi wakubwa sana, lakini ukija kuangalia the fact that hata hao business people ni consumers in one way or another, utaona ulipaji kodi kwa ni mkubwa kuliko low income earners kwa sababu, high income earners ndio maspender wakubwa sana and the higher you sepend the higher you pay tax!
Hayo ndio maoni yangu! Need more?