Popo kuingia ndani ya nyumba usiku ni uchuro?

kinywanyuku

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2015
Posts
3,746
Reaction score
2,924
Wakuu kuna imani eti popo akiingia ndani kwenu usiku na kuzunguka zunguka juu ya paa ni uchuro?

Kuna jamaa nilienda kwao wiki mbili zilizopita popo akaingia akazunguka ndani kama dakika kumi jamaa akaniambia uchuro kuna msiba utatokea. Leo kafiwa na baba yake mzazi huyo jamaa maana me hizi imani zao sizielewi
 
Kwenye maisha yangu hadi waleo nimekishuhudia hicho kitu mara nyingi sana kiasi huo uchuro ungekuwa umenizunguka kila kona.
 
Popo anazunguka kwenye nyumba furanifurani vijijini kwakuwa anakamata mbu.
Mbu ni kati ya vyakula vya popo, kwahiyo hakuna uchuro
 
Ndio nyinyi mnaoona bundi ni mchawi anapozunguka usiku, kumbe maskini bundi ni mla panya/panya buku na usiku ndio anawawinda majumbani kwenu wanaoranda randa nje au wanaotaka kuingia ndani...
 
Mbona nyumba nyingine popo wanaishi humo humo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…