The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Tume ya Ulaya imezitaka tovuti tatu kubwa zaidi za video za ngono duniani kutoa maelezo kuhusu hatua walizochukua ili kulinda watoto dhidi ya kufikia maudhui yao na kuzuia ukatili wa kijinsia.
Uamuzi huo umechukuliwa ili kuzilenga kampuni za Pornhub, XVideos na Stripchat chini ya Sheria ya Huduma za Kidijitali, au DSA, ambayo inaweka masharti madhubuti yaliyokusudiwa kuhakikisha usalama wa watumiaji wa mtandao. Kampuni hizo zinakabiliwa na faini iwapo hazitatoa taarifa ifikapo Julai 4.
Pornhub, XVideos na Stripchat zimewekwa katika kundi la “majukwaa makubwa sana ya mtandaoni” yanayokabiliwa na udhibiti mkali zaidi chini ya, Sheria ya Huduma za Kidijitali kwa sababu kila moja lina wastani wa watumiaji milioni 45 kwa mwezi.
“Tume inaziomba kampuni hizi kutoa maelezo ya kina zaidi kuhusu hatua walizochukua kutathmini kwa umakini na kupunguza hatari zinazohusiana na ulinzi wa watoto mtandaoni, pamoja na kuzuia kuenea kwa maudhui haramu na vurugu za kijinsia,” Tume ya Ulaya ilisema Alhamisi.
EU inataka kujua ni aina gani ya ulinzi zimewekwa kuhakikisha kuwa watazamaji si watoto. Katika majukwaa mengi ya ponografia, kubofya tu kwenye kisanduku cha “ndiyo” kinachosema mtumiaji ana umri wa miaka 18 au zaidi kinatosha kuingia.
Tume ya Ulaya pia inaziomba kampuni hizo kueleza jinsi zilivyobadili muundo wao wa ndani ili kuzingatia Sheria hiyo.
Mwaka jana, Pornhub ilipinga hadhi yake kama “jukwaa kubwa sana la mtandaoni” chini ya Sheria ya Huduma za Kidijitali, ikirejelea taarifa kwenye tovuti yake ikisema ina wastani wa watumiaji milioni 33 kwa mwezi.
Ufaransa, Ujerumani na Uingereza pamoja na majimbo ya Marekani, ikiwa ni pamoja na Utah na Texas, yameandaa sheria zinazohitaji tovuti za pornography kuthibitisha kuwa mtumiaji ana umri wa miaka 18 au zaidi. Njia zinaweza kujumuisha kukagua kadi za mkopo au kitambulisho kilichotolewa na serikali au kuchanganua nyuso ili kukadiria umri, lakini mifumo yote hiyo imeibua wasiwasi kuhusu faragha na ubaguzi.
Sheria ya Huduma za Kidijitali ya Ulaya inataka hatua za kudhibiti hatari ya kuenea kwa maudhui haramu mtandaoni, kama vile maudhui ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto, au maudhui yanayokiuka “haki za msingi” kama faragha, kama vile picha za bila ridhaa au ponografia za deepfake.