Porojo za Bongo

Bwana Bongo

Senior Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
146
Reaction score
212
porojo za bongo

"kaka maisha magumu hayaeleweki?
"hayaeleweki na hautayaelewa
"kwanini unasema hivyo kaka?
"kwasababu hayaeleweki
"sijakuelewa kaka unani acha mbali?
"lazima nikuache mbali sababu hutaki kunielewa
"kivipi kaka mbona unazidi nichanganya
"unajua kwanini nakuchanganya?
"sijui ndo nataka nijue
"kwasababu umeniweka kundi moja na maisha

bwana bongo ikabidi anyamaze sasa na kuvuta pumzi
"sikia nikwambie ndugu yangu"
alinitazama
"kule pande za kujidai za wachaga moshi, kibosho, machame,kibororoni, wanakauli inasema"
bado aliendelea kunitazama
"tuliza mtori nyama ziko chini" hakunielewa kabisa bado alinitazama niliendelea
"sasa wewe ukijifanya unapingana na hawa ndugu zangu wa moshi ukaanza uchokoa chokoa uwo mtori hautaufaidi"
"hautuache uko nikamkatiza juu juu"
akatumbua macho nakutikisa kichwa chini juu eti kujifanya ameleewa huyu ndugu yangu huyuu, wakati sasa hivi katoka kusema maisha hayaeleweki sasa sijui yeye kiujumla haya anaona ni nini labda ugoro au?

na mimi nikamtazama tu kisha nikaendelea kwa kuwa ameonesha kunielewa tutaelewana tu.

"sasa njoo kwa hawa ndugu za wa msanga, chole ,kule mwisho wa upepo vikumburu, njoo kidogo hapa kisarawe ,pandisha kwa juu pale kazi mzumbwi, awa ndugu yangu bongo wamejaliwa (mbuli kumlomo) watakunyima ugali lakini si maneno wanakwambia haraka haraka haina baraka, hawa hawa tena awaja maliza walivyo jaliwa maneno awakuishia hapo wakaongezea kwamba kila mwenye subra basi lazima amvute heri"
alitoa tabasamu hilo na kunionesha mipengo yake kabla ya kumnunisha na kauli
"sasa na mashaka na wewe inawezekana wewe ndio hueleweki na sio maisha"
"hizo zalau sasa "
"sio zalau maisha ni kama kibiriti kilicholoa wakati ambao hakuna uwezekano wowote wakupata chengine utafanyaje?
"aah ndugu yangu " eti ananizodoa
"si unarudi tu kwa hawa wazee wa mbuli kumlomo
"kwamba ??
"unamchukua subira unamuweka pale heri atakuja mwenyewe..
"ewaaaa"

#wamakamo
 
Bangi za kuvutia chooni hazijawahi kumuacha mtu salama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…