Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
UGOKO AIMWAGA KLABU YA WAPAMBANAJI
Ugoko aliogopa umande: Alikimbia shule na kuingia kwenye uchuuzi wa samaki akiwa kijana mdogo. Baadae alipobaini kuwa ana kipanji cha kunengua, aliacha biashara ya samaki na kuwa mcheza shoo kwenye mabaa mbali mbali. Mwenyewe anadai, pesa za kutunzwa na walevi ilikuwa ndefu kuliko faida ya samaki. Leo ni kingozi wa Taifa la Makeke!
Ni lazima tumpongeze Ugoko; kutoka kwenye unenguaji hadi siasa na hatimae urais wa taifa kubwa kama Makeke, inahitaji kipaji cha hali ya juu.
Kwenye kampeni zilizompa ushindi, Ugoko alipata kura nyingi toka kwa wazazi masikini waliovutiwa na sera yake ya kuokoa pesa za karo kwa kutopeleka watoto shule. Kauli mbiu yake ya, “Pambana Kitaeleweka”, ndiyo iliyochochea vijana wengi kuacha shule na kujiunga na upambanaji.
Siku mbili tu baada ya kuingia ikulu, alimwamuru waziri wa elimu kuondoa methali ya, “Elimu ni Ufunguo wa Maisha” katika orodha ya methali zinazofundishwa shuleni. Alidai methali hiyo inawatia ujinga watoto.
Sasa juzi vyombo vya habari vimetuletea habari ya kurusha roho kidogo: Ghafla tu, Ugoko ameripotiwa kutunukiwa PHD ya heshima na chuo kimoja cha huko majuu! Walio karibu naye wanasema, tangu juzi, amekuwa mkali sana kwa watu wanaozungumza na kufanya mambo kama hawajaenda shule. Wapambanaji wanadai hii habari imewaacha kwenye mataa!
#MimiNaSiasa