Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kuna watu na mataifa yanayoizunguka Kenya wanapenda sana kujijaza upepo na kujifariji ili mambo yanavyofanyika na hali za nchini mwao yaonekane mazuri.
Siasa na Ukabila
Siasa za Kenya sio za Ukabila bali za maslahi na jiografia.
Watu wanaofanya biashara wanapenda siku zote kuwakilishwa katika ngazi muhimu na mtu anayefanya au kuelewa vizuri biashara kama wao. Wakulima mara nyingi hupenda mfanyabiashara awawakilishe na mara nyingi pia mkulima huwa mfanyabiashara
Wafugaji siku zote wanapenda kuwakilishwa na mfugaji mwenzao au mtu anayelewa mambo na maslahi yanayohusu ufugaji.
Haya ndio makundi ambayo mara nyingi yanaamua siasa za Kenya, maeneo na makabila yanaingia humo ila sio karata turufu. Wakenya wanachangamana vizuri sana kwa makabila yao tofauti bila ubaguzi wowote.
Umaskini
Kuna porojo huwa zinasambaa sana mitandaoni kusema hali ya umaskini Kenya ni ya kutisha. Sio kweli, Kenya ina asilimia chache ya maskini kuliko nchi zote za Africa mashariki kwa 17% ya raia wake
Chakula
Kenya haina shida au njaa ya Chakula, kuna watu wanafikiri Kenya kununua chakula nchini za jirani ni sababu ya matatizo ya Kilimo. Sio kweli, sababu ni pesa waliyo nayo.
Njaa inaletwa na ukosefu au uduni wa kipato.