Posho kwa waajiriwa kwenye maduka ya hardware(construction material)

Posho kwa waajiriwa kwenye maduka ya hardware(construction material)

Mkuu shukuru Mungu umepata kazi.

Usiwaze sana kuhusu marupurupu maana itakupelekea kwenye hatua ya udokozi na tamaa.

Fanya kazi, riziki itakuja na hayo marupu rupu yatakuja katika namna ya pekee.

Ukianza mawazo ya posho, utaiba siku sio nyingi.

Jiulize kabla ya wewe kupata hiyo ajira, huenda kuna mwingine alikua anafanya kazi hapo, je nini kilimkumba mpaka wewe uitwe?
 
Wakuu nimepata ajira ya kuuza hardware dar kariakoo ila mshahara ni laki 3 kwa mwezi.
Nilikuwa naomba kuuliza kwa yeyote mwenye uwelewa na hii kazi ya hardware huwa inamarupu rupu?
Shinda hizo tamaa ulizo nazo vinginevyo hutadumu hapo kazini. Fanya kazi kwa uaminifu na ridhika na mshahara wako. Marupurupu ni neno linalotumika badala ya wizi, ubadhirifu na udokozi maeneo ya kazi. Futa neno marupurupu kwenye ubongo wako. Pia ACHA TAMAA
 
Hutu ndiyo tutoto twa humu jamiiforums kila siku tunaomba kazi ukitupa kazi ,tunaanza kuwaza posho ilihali kazi haina makubaliano ya posho .

Hutu unatuacha tuibe finally unakazima mshahara hata wa mwaka kakawasimulie wanakijiji huko kwao
 
Unataka ushauriwe uibe sio?

Bure kabisa.

We umeandikwa kazi na mtu huko kariakoo unakuja kutuliiza posho JF? Tutajuaje makubaliano yenu?

Yaani mmekaa kiwizi wiziiiiiii
 
Mwajiri wako kama yupo humu awe makini na wewe, hizi nyuzi zako ni dhahiri hujaridhika na mshahara.

Ingia mjini vizuri kijana, makinika.
Ni kazi nzuri ila usipokua makini itakupoteza.
 
Mliojibu swali wote hamjielewi, rudieni kusoma swali then mjibu uzi kazi kukurupuka tu
 
Hiyo kazi ina marupurupu sana mkuu! Ndugu yangu alikuwa anaifanya hiyo kazi! Alikuwa hana shida na mshahara wake! Ukiwa mnjanja ila sio wizi kuna hela sana!
 
Back
Top Bottom