desertfish
Member
- May 25, 2009
- 21
- 1
agenda kubwa kwa spika sita ni kuwapendeza wabunge kwa maslahi. mishahara, posho, fungu la la majimbo nk. sasa pia anapigia debe posho mbili mbili na kuziita ukarimu wa kiafrika. masikini kukarimu matajiri kwa posho za kimtindo ambazo nazo kwa kawaida ni zaidi ya posho za bunge.
kwa kuwapendelea wabunge kwa maslahi yao binafsi anadhani hawezi kung'olewa ubunge.
macinkus
nilimwamini, nikamkubali, nikasema tumepata jasiri wa kusema kwa ajili ya wanyonge. Akaanza kwa mbwembwe za speed and standard,akatetea nyongeza ya mishahara ya wabunge,akasemwa,akatulia!
Lakini kwa namna anavyoshughulikia swala la richmond, halafu hashughulikii mengine kwa kasi hiyo, napoteza imani nae. Kama vile ana kisasi flani. Mbona kagoda haiundiwi tume? Meremeta? Tangold?
Mbona anatetea sana wabunge hata kwenye mambo ambayo yanaonekana wazi yanahitaji kuguswa?
Mbona ikiguswa ofisi yake anageuka mbogo? Au milioni sabini ni hela za chai kwake? Haoni kama zingewaletea maji wamasai wa ngorongoro? Mbona ofisi yake ikiguswa anawaka wakati ye ndo kinara wa ufisadi?
Kwa haya na mengine mengi, napoteza imani na huyu bwana, nadhani ndo maana wakina el na ra kila siku wanawaza kumpindua
Kwa mara nyingine Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Samwel Sita amezungumzia suala la Wabunge kulipwa posho zaidi ya moja kwa kuunga mkono Wabunge kupokea posho zaidi ya moja kwa kazi ile ile! Alisema wanaozungumzia suala hilo waonane nao majimboni na wanawaonea wivu! Cha kujiuliza ni kwamba kama Spika Sita aliwataka Wabunge wakahojiwe huku anaunga mkono wabunge hao kulipwa posho zaidi ya moja, sasa aliwataka wakahojiwe kuhusu nini? (Source: www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=15648).
Kipengele kipi kna halalisha posho hizo na kwa PCCB ni kipengele kipi ninazuia posho mbili ?
Buchanan,
Mkuu ubadhirifu huo ni baada ya mkaguzi wa mahesabu kutoa taarifa yake..PCCB hawawezi kufuata sheria hiyo ikiwa hakuna ushahidi tosha na sio kuutafuta ushahidi ktk kosa ambalo hawajui kama lipo au halipo.
roho inaniuma sana jamani, Viongozi wanapotetea ujinga. Ndio maana gap between rich and poor linazidi kuongezeka. Hizo 6.9 m hapo bado hajalipwa mshahara, na posho hazijalipwa marahaba mbili! du!?!ukiongelea mshahara wa mwalimu, hiyo ni topic nyingine ambayo mmh, acha tu.
Ndugu zangu lazima kila kitu kiwe na mwanzo wake. Kama kuna udanganyifu unafanywa na wabunge uanikwe na ukemewe. Kama wabunge is mafisadi kwanini wagushi risiti? Kwanini walipwe mara mbili kwa kazi moja? Wanaosema kwamba ni kwa sababu ya wao kuibana serikali kuhusu Richmond haina mantiki yoyote. Wote wanaohisiwa wahojiwe na wale watakaokua na hatia warudishe hizo hela zetu na wengine ikibidi waburuzwe mahakamani. Baadhi ya wabunge wanaficha maovu yao kwenye kivuli cha kupambana na ufisadi.
Dr. Slaa alishalalamika hili juu ya mapato makubwa ya wabunge.