Posho ya chakula na malazi ya wanavyuo imeongezwa migomo itaisha vyuoni?

Posho ya chakula na malazi ya wanavyuo imeongezwa migomo itaisha vyuoni?

potokaz

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2011
Posts
540
Reaction score
493
Shukuru kawambwa yuko hewani, anawasilisha bajeti ya elimu, habari njema kwa wanavyuo, posho imeongezwa toka elfu tano hadi elfu saba mia tano!. Migomo itakwisha vyuoni?
 
Issue sio kuongeza pesa, Issue ni Je hizo pesa watazilipa kwa wakati???!!. Kwa sababu Migomo mingi ya hawa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu inasabishwa na Kucheleweshwa kwa hizi pesa kuwafikia Wanafunzi on Time.
Tuache Siasa, kama Serikali imekubali kuwasomesha hawa Wanafunzi, basi ikubali pia kuwapatia fedha kwa wakati muafaka
 
Mtoto wangu anaenda field mwezi wa July 2011
amepewa sh 1000 eti ndo allowance ya chakula, hii serikali haiko serious kabisa
 
Kama dhuluma bado zipo kwa wanafunzi migomo haiwezi kwisha,kuna pai mazingira bora ya kusomea,vitabu (library) etc etc.
 
2nasubiri udsm wagome,c walikua wanataka elf 10?
 
Ako kaela bado ni kadogo mno,hakatolewi kwa wakati,wanalala vitanda havitoshi,wanaoishi mtaani kodi inaongezeka,wanafunzi wanakopeshwa lakini bado wanatengewa pesa ndogo hivi ilihali wanaoitenga hela hii wao walisoma kwa hisani bure na bado leo wanakomaa kuongezewa posho zao eti 150,000 kwa siku haiwatoshi,kwa inequalities hizi badala ya kupungua kwa migomo nahisi itaongezeka zaidi
 
Kwa kweli maisha yamepanda ila angalau wamejitahidi kupandisha ila waboreshe na taratibu za bodi ya mkopo ili mkopo iwahi wanavyuo watulie wasome 2pate magraduates bora na sio bora graduates!!
 
Mtoto wangu anaenda field mwezi wa July 2011amepewa sh 1000 eti ndo allowance ya chakula, hii serikali haiko serious kabisa
u cant be seriouz mkuu,ina maana ana asilimia ngap ya mkopo hadi apewe hyo buku?
 
Bodi ya mikopo ina mapungufu makubwa sana ila sishangai kama waliweza kumlipia jamaa ada toka tuko 1st hadi 3rd na allowance kibao za magraduate wakati alifariki tukiwa 1st semester 1st year,ila kuhusu ongezeko la posho tunashukuru kama ni kweli ila in economics tunaambiwa HUMAN NEEDS ARE INSATIABLE hata wadogo wangepewa 100,000 migomo itabaki palepale either coz gharama za chuo zitapanda or matatizo tu ya wadogo wanapotaka kupata mapumziko katikati ya semester
 
pongezi kwa wizara ya elimu kwa kuongeza posho za wanafunzi lakini napenda pia kuilamu kwani kiwango hicho bado hakitoshi kwani gharama za maisha zimepanda vyuba kwa sisi tunaoishi of compus vina bei ya juu, hivyo mi nahisi migomo haita isha mpaka pale haki itakapo patikana, pia kwa upande mwingine utekelezaji wa utoaji mikopo bado dhaifu mfano mpaka sasa idadi kubwa ya wanafunzi hatuja pata pesa ya field, kwa kuishauri serikali naona bodi ya mikopo ivunjwe na iundwe mpya ambayo itatetea maslahi ya wanafunzi na sio kuunda tume ambazo majibu ya uchunguzi wake hayawekwi hadhalani
 
49% ya bajeti ya wizara ya elimu ni kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu
 
Wacpo nilipa kwa wakat nagoma kama kawa!
Sasa ndio watachoma mavasitiz baada ya kilaji. They were thinking small in thuggery move after being made high, they (our scholars) will think big in that arena.
 
Kwa kweli maisha yamepanda ila angalau wamejitahidi kupandisha ila waboreshe na taratibu za bodi ya mkopo ili mkopo iwahi wanavyuo watulie wasome 2pate magraduates bora na sio bora graduates!!
Wamesema wataiboresha bodi ya mikopo kwa ajili ya kukopesha kwa wakati mwafaka na kufuatilia marejesho ya mikopo kwa wakati mwafaka. Labda kama ni politics tu.
 
Shukuru kawambwa yuko hewani, anawasilisha bajeti ya elimu, habari njema kwa wanavyuo, posho imeongezwa toka elfu tano hadi elfu saba mia tano!. Migomo itakwisha vyuoni?
migomo km kawa wanavyuo wanataka tsh 10,000 na sim 75,000.
 
kama kawa,hiyo ni kawaida ye2 chalii yangu.
hawa jamaa porrrojo nyingi sana,kama unasoma ud ina takiwa upange karibu,na nyumba za karibu hyo mikodi yakeee,la cvyo ukapange huko mbagala makamasi chumba buku10 no maji no umeme...af nauli zake utakoma!
 
Tunataka 10,000/=! Si tutazilipa, kwan tatzo nini? Mbona wenyewe wanakamua hela ndefu halafu hawarudish? Wap mahela ya EPA,RADA?
 
Back
Top Bottom