Posho ya wanafunzi wa elimu ya juu yaongezwa hadi Tsh.7500 kwa siku.

Posho ya wanafunzi wa elimu ya juu yaongezwa hadi Tsh.7500 kwa siku.

The Magnificent

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
2,694
Reaction score
1,249
Hatimaye wizara imeongeza posho ya wanafunzi wa elimu ya juu kutoka sh.5000 hadi 7500.
Source:bungeni-dodoma,leo.
 
Ni jambo jema,ila wanafunzi inabidi kuwa makini katika matumizi yao otherwise wataendelea kulia njaa daily.
 
Vyakula vitapanda na gharama ya malazi itapanda pia hivyo wanavyuo watabaki pale pale walipokuwa.

Nyongeza inakuwa faraja ya mamantilie wanaopika vyuoni mfano pale Mzumbe (Wakuu msinirushie vijembe tafadhali!).
 
Mhh hakuna kitu hapo. Wanafunzi waliomba nyongeza ya 100% ili posho kufikia shilingi alfu kumi. sasa serikali imetoa 2500!!! Mhh mi nafikiri ni chanzo kingine cha migomo maana ongezeko halikidhi hali halisi ya kupanda kwa maisha. Kama wabunge wanapata shilingi alfu 80 kama perdiem yao na bado wanasema hazitoshi leo hii mwanafunzi anapata hiyo 7500 kwa siku, Ale, alipie pango, na matumizi mengine kweli???? Ngoja tuone.
 
Kwa ughali wa maisha ya sasa bado ni peanut!
Imagine mtu yuko ifm pale unampa iyo ela si itaishia kwenye chakula tuu!
Haya mahesabu yao bench mark huwa wapi?
 
maoni yangu: wangeanza kuwafikiria wafanyakazi wa serikalini kwanza kupunguza rushwa na ukali wa maisha ukizingatia wao wana familia, wanasomesha, kodi ya nyumba, chakula etc hawa wanafunzi wangewaacha kwanza
 
kwa hali hii ya maisha?! Tutaona kama migomo itafika kikomo! 7500 haitoshi banaa!
 
juhudi wap wkt cku ya mgomo ulijifungia chumban,wkt wanaume wanakutetea
we njoro vp,bila udsm huko muccobs kwenu mtanyimwa haki zenu nying,so jarbu kuonyesha heshma kdogo kwa wasomi wa ud!
 
vipi ili swala kibonde kashalisikia au ndo bado haja liona..
 
tayari wahindi wa st joseph college wameshapandisha ada ya mitihani na kuweka sheria mpya, anaeshindwa kuchomoa sup alipe asilimia 10 ya ada kwa kila somo. Means laki 2 na 70 kwa somo
 
Hatimaye wizara imeongeza posho ya wanafunzi wa elimu ya juu kutoka sh.5000 hadi 7500.
Source:bungeni-dodoma,leo.

Haya mkapige exile na viroba..mnadhani hatuwajui..tena siku hz mnapiga valuer..
 
Back
Top Bottom