Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mwamuzi wa Ligi Kuu anapokuwa kwenye mechi, inaelezwa analipwa kati ya Sh 300,000 hadi 350,000 kwa mechi, pesa ambayo inajumlisha nauli ya kutoka anakoishi kufika kwenye kituo cha kazi na gharama za malazi na chakula.
🗣 Ukipiga hesabu kwa haraka haraka, pesa ya posho kwa mwamuzi wa Ligi Kuu inaweza kufika gharama ya vitendea kazi vyake vyote anavyopaswa kuwa navyo.
Mfano gharama za kiatu kwa mwamuzi, kuwa cha bei ya chini uwa ni Sh 45,000 na kile cha bei kubwa ni Sh 120,000, lakini pia jezi ambayo moja ni Sh 25,000 mara nne, hivyo laki moja.
.
Kibendera ni Sh 35,000, kuna filimbi ambazo zinahitajika kuwa tofauti tofauti ili ikitokea mashabiki wana filimbi yenye mlio kama wa mwamuzi inabidi uweze kubadilisha, kadi na vifaa vingine vinavyohitajika kwa waamuzi.