Posho za marefa Ligi kuu ni huzuni

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610

Mwamuzi wa Ligi Kuu anapokuwa kwenye mechi, inaelezwa analipwa kati ya Sh 300,000 hadi 350,000 kwa mechi, pesa ambayo inajumlisha nauli ya kutoka anakoishi kufika kwenye kituo cha kazi na gharama za malazi na chakula.

🗣 Ukipiga hesabu kwa haraka haraka, pesa ya posho kwa mwamuzi wa Ligi Kuu inaweza kufika gharama ya vitendea kazi vyake vyote anavyopaswa kuwa navyo.

Mfano gharama za kiatu kwa mwamuzi, kuwa cha bei ya chini uwa ni Sh 45,000 na kile cha bei kubwa ni Sh 120,000, lakini pia jezi ambayo moja ni Sh 25,000 mara nne, hivyo laki moja.
.
Kibendera ni Sh 35,000, kuna filimbi ambazo zinahitajika kuwa tofauti tofauti ili ikitokea mashabiki wana filimbi yenye mlio kama wa mwamuzi inabidi uweze kubadilisha, kadi na vifaa vingine vinavyohitajika kwa waamuzi.
 
Mwamuzi wa Ligi Kuu anapokuwa
kwenye mechi, inaelezwa analipwa kati ya Sh 300,000 hadi 350,000 kwa mechi, pesa ambayo inajumlisha nauli ya kutoka anakoishi kufika kwenye kituo cha kazi na gharama za malazi na chakula...
Mkuu unataka kumaanisha kila mechi atakayochezesha mwamuzi anaingia gharama mpya ya kiatu, jezi, kibendera na filimbi?
 
Mwamuzi wa Ligi Kuu anapokuwa
kwenye mechi, inaelezwa analipwa kati ya Sh 300,000 hadi 350,000 kwa mechi, pesa ambayo inajumlisha nauli ya kutoka anakoishi kufika kwenye kituo cha kazi na gharama za malazi na chakula...
Waamuzi wengi wa tz ni waajiriwa wa serikali baadhi yao ni maasilkari jeshi polisi na n.k

So wanamishe nyingine ila posho hiyo sio haba.. kama unamatch 4 kwa mwezi sio mbaya..
 
Kwahiyo pesa aisee ni rahisi kuwapa milion moja wakagawana na mkapata penati za mchongo na maisha yakaendelea na bado tukamuita nabi professor
 
Mwisho wa siku, posho ziongezwe ili hao waamuzi wachezeshe kwa weredi, na pi kwa kufuata sheria 17 za mpira wa miguu. Laki 5@mechi siyo mbaya.
 
Hapa Tz kazi gani nyingine ambayo ndani ya dk 90 mtu analipwa tshs 350000?

Tunadharau vitu wakati tunajua posho za hapa Tz zilivyo ili iweje? Tukumbuke ni waamuzi wengi pia huchezesha mechi moja that means kuna uwezekano mkubwa matumizi kwa mechi za siku moja TFF inatumia more than 20 milions sssa jaribu kuipiga kwa mechi za msimu mzima uone ni sh ngapi

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…