Posho za watumishi zilizofutwa na Serikali ni zipi?

Leverage

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2021
Posts
2,125
Reaction score
3,150
Jana tarehe 19/7/2021 katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV, Waziri Mwigulu akihojiwa na Farhia Midley:

Swali: Mnataka wananchi wafunge mikanda lakini nyinyi viongozi hamuonekani kufunga mkanda"

Jibu: "Kutokana na serikali kuwa serious na swala la kubana matumizi imefuta posho zote za watumishi na viongozi ili fedha hizo zikafanye shughuli za maendeleo"

Je, hili swala linawezekana kweli au ni kwenye media tu.

Ni posho gani zilizofutwa na serikali?
 
Sio rahisi kufuta Posho zilizowekwa kisheria.

Mfano unawezaje kufuta posho ya safari (Per-diem) ili hali unajua Mtumishi hana nyumba wala hotel ya yeye kwenda kula na kulala bure awapo na safari ya kikazi.

Vinginevyo labda kuwe na hotel za watumishi kila Mkoa na Wilaya za wao kwenda kula na kulala bure kila wanapokuwa na semina maeneo hayo.
 
Au ndio kujisafisha machoni pa walalahoi
 
Anajaribu kujisafisha kwa walalahoi ili hali ni juzi tu hapo yeye mwenyewe amejilipa posho ya 300,000 kwa siku alipokuwa Bungeni akihitimisha Bajeti yake ya Wizara ya Fedha!
 
Amesema hana mamlaka ya kubatilisha maamuzi ya Bunge, hizo posho ana mamlaka ya kuzifuta
 
Jana tarehe 19/7/2021 katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV, Waziri Mwigulu akihojiwa na Farhia Midley:

Swali: Mnataka wananchi wafunge mikanda lakini nyinyi viongozi hamuonekani kufunga mkanda"

Jibu: "Kutokana na serikali kuwa serious na swala la kubana matumizi imefuta posho zote za watumishi na viongozi ili fedha hizo zikafanye shughuli za maendeleo"

Je, hili swala linawezekana kweli au ni kwenye media tu.

Ni posho gani zilizofutwa na serikali?
Ameropoka
 
WAKATI WA MPANGO BADO MLILALAMIKA..SUALA LA TOZO BADO LIBAKI ILA KWA MIAMALA YA CHINI YA ELF LAKI WALIPE 30% YA SASA ..HARAFU ZAIDI LAKI MOJA HADI 4 WALIPE 50%YA SASA HARAFU ZAIDI YA HAPO TULIPE KAMA ILIVYOSASA.Hii inamfanya kila mtanzania kuchangia kidogo kwa chochote alichajiliwa ili tujenge barabara vijijini na mashuoe ya secondary..Bila kufanya hivi kodi ya bidhaa haitoshi
 
Jana tarehe 19/7/2021 katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV, Waziri Mwigulu akihojiwa na Farhia Midley:

Swali: Mnataka wananchi wafunge mikanda lakini nyinyi viongozi hamuonekani kufunga mkanda"

Jibu: "Kutokana na serikali kuwa serious na swala la kubana matumizi imefuta posho zote za watumishi na viongozi ili fedha hizo zikafanye shughuli za maendeleo"

Je, hili swala linawezekana kweli au ni kwenye media tu.

Ni posho gani zilizofutwa na serikali?
Uliona wapi mtu mwenye akili timamu akichora mawe mjini kama ana PhD? Alichokisema potezea
 
Anajaribu kujisafisha kwa walalahoi ili hali ni juzi tu hapo yeye mwenyewe amejilipa posho ya 300,000 kwa siku alipokuwa Bungeni akihitimisha Bajeti yake ya Wizara ya Fedha!
Tanzania bado sana
 
Jana tarehe 19/7/2021 katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV, Waziri Mwigulu akihojiwa na Farhia Midley:

Swali: Mnataka wananchi wafunge mikanda lakini nyinyi viongozi hamuonekani kufunga mkanda"

Jibu: "Kutokana na serikali kuwa serious na swala la kubana matumizi imefuta posho zote za watumishi na viongozi ili fedha hizo zikafanye shughuli za maendeleo"

Je, hili swala linawezekana kweli au ni kwenye media tu.

Ni posho gani zilizofutwa na serikali?
Watanzania sio mazezeta. Kama kuna posho zimefutwa itakuwa kwa watumishi wadogo wadogo tu.Hii michwa(mchwa)bado ina utitiri wa posho. Posho za mafuta ya gari, vocha za simu,nyumba, vikao, safari za kikazi, posho za makalio(sitting allowances),kwa kutaja baadhi tu. Hebu wajaribu kuishi kama watumishi mfano walimu ambao hutegemea mshahara kwa 100%.
 
Back
Top Bottom