Post ya mwanamke na comments za wanaume

Deadbody

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2015
Posts
4,274
Reaction score
6,595
UKIWA FACEBOOK kuna mambo noma sana. MWANAMKE anajiita Cuttly beibz Pweeery Libs ameposti: "Uwiiiiiiiii" na ndani ya 5 minutes kuna 'like' 200 na 'comment' 140. Kwenye hizo komenti humo ndani masela wanagombea kucomment hadi wanaanzishiana bifu kinyama mpaka wanatukanana mama na dada zao!

MWANAUME mstaarabu anajiita Jastin anaposti: "Mchana Mwema Rafiki zangu, YESU awasimamie kwenye kazi zenu, Nawapenda sanaaa Rafiki zangu!" na ndani ya masaa 10 kuna 'like' 3 na 'comment 2. Comment zenyewe masela wanamponda, "Acha ufala wewe hapa sio Kanisani Unajifanya Mchungaaaaajiiiii!"

Buhahahahaha kwa namna hii kweli acha wanawake waringe tu. Facebook bwana! Ndio maana mimi, HATA KWENYE MAISHA HALISI, sishindani na mwanamke hata kidogo.
 

Mkuu pure math, hao ni wanawake wa 20-24 baada ya hapo soko hufa na kubaki kupost namtegemea Mungu wewe fanya research kidogo utaona
 
Huu uzi umeanzishwa jana lakini hadi sasa comments ni za manati,...angekuwa kaanzisha demu, hali ingekuwa tofauti.
 
Mkuuu wee face book unatumia jina gani!!
 
hapo colored nimecheka mno
Hii hali ni kweli mkuu...nenda kule MMU au Love connect ujionee nyuzi zinazo anzishwa na KE alafu ulinganishe na zile za ME ni kitu tofauti kabisa, yaani unakuta ME ana mada nzuri ila anapewa maneno ya kashfa kwenye comments kama....Chuo kimefunguliwa?......kizazi cha mwendo kasi....peleka hizi pumba FB au Insta.....Hadithi za kutunga peleka bongo movie.

Lakini kama amepost KE, hata kama ni mashudu utaona mijitu inaanza....Mkuu njoo PM tuyajenge, na maneno kibao ya kujikomba....huu ni ujinga wa hali ya juu.
 
halafu mademu wa mtandaoni wengi wabaya,picha mpaka ikaende hewani imepitia photoeditors kama nane,
na wanaume wengi wanao comment sana kwenye picha za mademu wengi ni madomo zege fanya research
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…