Post za walimu wapya,je serikali imefilisika?

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2013
Posts
22,532
Reaction score
6,624
Ndugu wana jf nadhani mu wazima wa afya. Kama mjuavyo suala la serikali kuajiri watumishi wapya wakiwemo walimu limezungumzwa tangu muda mrefu na viongozi mbalimbali wa kisiasa tangu mh. Rais kikwete,waziri wa elimu na viongozi wengine waandamizi serikalini. Kuna taarifa zisizo rasmi toka serikalini kuwa serikali haina pesa za kuajiri watumishi wapya,ingawa madai haya yamekuwa yakipingwa kwa nguvu zote na mawaziri wa serikali hii ya jk. Je nini sasa kinachochelewesha serikali kuajiri walimu wapya ili kuondoa upungufu wa walimu katika mashule ya umma? Je kauli za viongozi wa kisiasa kuwa serikali imeshaajiri walimu wapya ilikuwa ya kisiasa? Je huu ni mwendelezo wa ghiliba ya serikali hii ya ccm? Kwa watanzania? Je kulikuwa na ulazima wa suala hili kulitangaza kwa umma kabla ya kujipanga? Karibuni.
 
Serikali inayopenda sifa,wakati uwezo ni mdogo. Ccm wanafanya mambo kinyume na sera yao ya ujamaa na kujitegemea.wanataka kuajiri walimu mpaka wapate msaada toka nje. Hayo ndo maisha bora kwa kila mtanzania!
 
kuwa na subira ndugu yangu.waliahidi zitatoka januari hii.najua ni ukata unaokusumbua ndo mana unaona zinachelewa.
 
Kwani madarasa hayapo? Wanafunzi hawahudhurii darasani?,magogo ya kukalia darasani hayapo? Jibu ni kwamba serikali sikivu imejenga madarasa ya kutosha,kila kata ina shule angalau moja ya sekondari. Watanzania wenye umri wa kuhudhuria shule wanatekeleza jukumu lao. Madawati ya asili yapo nchi ina miti ya kutosha. Kwa tanzania walimu sio kipaumbele
 
Hilo nalo ni lakuuliza,wafanyakazi waliopo inashindwa kuwalipa kwa wakati, unataka iongeze matatizo mengine?
 
ajira ya ualim kumbe dili eh...!ila ndo nyie chuoni mlikuwa mnaponda ati hata km mnasoma ualim hamtaenda kushika chaki.cku hz mnaulizia post kila cku.mkipangwa mkafanye kazi.isije kuwa mnapenda mishahara tu afu utoro kila cku.Nyooo...!Chezea Jobles ww?
 
umegonga penyewe mazazi... Wengi hutukana wakunga wakati uzazi ungalipo, maji yamewafika shingoni sasa hawana pakushika.
 
Ndugu wana jf nadhani mu wazima wa afya. Kama mjuavyo suala la serikali kuajiri watumishi wapya wakiwemo walimu limezungumzwa tangu muda mrefu na viongozi mbalimbali wa kisiasa tangu mh. Rais kikwete,waziri wa elimu na viongozi wengine waandamizi serikalini. Kuna taarifa zisizo rasmi toka serikalini kuwa serikali haina pesa za kuajiri watumishi wapya,ingawa madai haya yamekuwa yakipingwa kwa nguvu zote na mawaziri wa serikali hii ya jk. Je nini sasa kinachochelewesha serikali kuajiri walimu wapya ili kuondoa upungufu wa walimu katika mashule ya umma? Je kauli za viongozi wa kisiasa kuwa serikali imeshaajiri walimu wapya ilikuwa ya kisiasa? Je huu ni mwendelezo wa ghiliba ya serikali hii ya ccm? Kwa watanzania? Je kulikuwa na ulazima wa suala hili kulitangaza kwa umma kabla ya kujipanga? Karibuni.

tafuta tempo ndugu yangu,ukiisubiri hii serikali utapata presha bure!
 
ajira ya ualim kumbe dili eh...!ila ndo nyie chuoni mlikuwa mnaponda ati hata km mnasoma ualim hamtaenda kushika chaki.cku hz mnaulizia post kila cku.mkipangwa mkafanye kazi.isije kuwa mnapenda mishahara tu afu utoro kila cku.Nyooo...!Chezea Jobles ww?

Usipende kujumuisha kundi la watu kwa msemo uliosikia toka kwa mtu mmoja wengine wanapenda ualimu toka moyoni na wanajisikia faraja na furaha tosha kuwaondoa watu ujinga hata kama ni kwa kujua KKK.
 
lazima utakuwa mwalimu wewe? Vipi wewe unaipenda toka moyoni?
 
Bora wachelewe ili hata zikitoka na pesa za kujikimu na mishahara iwe ishapatikana kuliko wazitoe sasa hv halaf tukaanze kuxota kwa ukata hko ktk vituo vya kaz, tutakimbiana jameni!
 
Back
Top Bottom