nkongu ndasu
JF-Expert Member
- Jan 19, 2013
- 22,532
- 6,624
Ndugu wana jf nadhani mu wazima wa afya. Kama mjuavyo suala la serikali kuajiri watumishi wapya wakiwemo walimu limezungumzwa tangu muda mrefu na viongozi mbalimbali wa kisiasa tangu mh. Rais kikwete,waziri wa elimu na viongozi wengine waandamizi serikalini. Kuna taarifa zisizo rasmi toka serikalini kuwa serikali haina pesa za kuajiri watumishi wapya,ingawa madai haya yamekuwa yakipingwa kwa nguvu zote na mawaziri wa serikali hii ya jk. Je nini sasa kinachochelewesha serikali kuajiri walimu wapya ili kuondoa upungufu wa walimu katika mashule ya umma? Je kauli za viongozi wa kisiasa kuwa serikali imeshaajiri walimu wapya ilikuwa ya kisiasa? Je huu ni mwendelezo wa ghiliba ya serikali hii ya ccm? Kwa watanzania? Je kulikuwa na ulazima wa suala hili kulitangaza kwa umma kabla ya kujipanga? Karibuni.