Mzito Kabwela
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 18,887
- 7,673
Hii ni SACCOS iliyoundwa na wafanyakazi wa mashirika ya Posta na TTCL. Inasemekana kuwa uongozi wa hii SACCOS umekuwa na matumizi mabaya ya fedha sambamba na wizi na ubadhirifu mkubwa kiasi kwamba imeshindwa kulipa malimbikizo ya michango ya wanachama waliojitoa kwenye SACCOS hiyo sambamba, walio staafu na waliofariki.
Taarifa zinadai kuwa wanachama hao kwa miaka minne mfululizo wamekuwa wakidanganywa kuwa SACCOS haina fedha huku ukweli ni kuwa fedha zipo lakini menejimenti ya sasa haina mpango wa kuwalipa wadai hao kwa kile kilichoelezwa hawahusiki na wizi uliofanyika siku za nyuma.
Wanachama wastaafu kadhaa niliobahatika kuzungumza nao wanasema SACCOS hiyo inaendelea kutoa mikopo kwa wanachama wachache waliobaki lakini hawana mpango kabisa wa kulipa madai wanayodaiwa.
Wapo waliofariki ambao wasimamizi wa mirathi wamekuwa wakipigwa 'njoo kesho' kila mara bila kujali wanatokea umbali gani na kila wakija wanakatazwa hata kuonana na meneja au hata mwenyekiti wa bodi ili waeleze vilio vyao.
Tayari mkakati wa kisheria unaandaliwa na baadhi ya wadai lakini hali ya wastaafu na wajane/wagane sambamba na waliojitoa uanachama ipo kwenye sintofahamu ya kujua lini watalipwa malimbikizo ya michango yao halali.
Wito umetolewa kwa Serikali kuingilia kati suala hili kabla ya mambo makubwa hayajajitokeza