Posta yajidhatiti kuimarisha huduma zake jijini Dodoma

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
POSTA YAJIDHATITI KUIMARISHA HUDUMA ZAKE JIJINI DODOMA.

Na mwandishi wetu- Dodoma

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Macrice Mbodo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Anthony Mtaka, kwenye Ofisi za Mkuu huyo wa Mkoa, Jijini Dodoma.

Kikao hicho kilichofanyika tarehe 28 Juni 2021, kililenga kueleza fursa mbalimbali na mikakati ya Shirika la Posta katika utoaji huduma kwa Mkoa wa Dodoma. Katika mazungumzo hayo Kaimu Postamasta Mkuu aliainisha namna Shirika lilivyojipanga kuwekeza na kushiriki katika maendeleo ya jiji la Dodoma, hasa kwenye nyanja ya usafirishaji, huduma ya duka la mtandao "Posta online shop", fursa za kupangisha kwenye majengo ya Shirika pamoja na huduma mpya ya "Posta Kiganjani" ambapo huduma za posta zitapatikana kupitia simu ya mkononi.

Katika kikao hicho Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma waliazimia kufanya ushirikiano wenye tija kwa Mkoa na namna ushirikiano huo utakavyoweza kuwanufaisha walengwa ambao ni Taasisi mbalimbali za kiserikali, Taasisi Binafsi, za Kiraia na Wananchi kwa Ujumla.

Imetolewa na:
Ofisi ya Mawasiliano
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.
[6/28, 6:15 PM] Samora Julius: POSTA YAJIDHATITI KUIMARISHA HUDUMA ZAKE JIJINI DODOMA.

Hivi hili Shirika bado ni "Posta na Simu" ?.
 
Ni kaimu posta masta mkuu, sasa aliyekua kua mkuu alienda wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…