Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Haihitajiki kusubiri Jumatatu ya October 26 kuanza kutafakari Uchaguzi wa 2015. Matokeo ya uchaguzi kwa sisi wengine si kigezo sana tena cha kuona ni upande gani wa njia panda tunachukua kama Taifa katika safari yetu.
Msisimko ulikuwa mkubwa sana, lakini je nia na dhamiri ya msisimko ni kutimiza wajibu na haki ya kikatiba au ndio taswira mpya ya kupotoka kwetu kama Taifa kuelewa dhamana na hatima ya kesho yetu kama Taifa?
Kushindikana kwa midahalo ya kutofautisha Sera, Itikadi na mipango kwa Taifa ni dalili tosha kuwa tumekwama keepleft au round about tunazunguka zunguka tuu, bila kujijua.
Hata katika hamaki yetu ya ukosefu wa heshima kwa katiba na kanuni za vyama (CCMChadema-Ukawa), bado uchaguzi huu tumeugeuza kuwa kituko, mashindano ya matusi, kubezana na sasa ni vitisho vya kutunishiana misuli kuitishia ile bahati ya mwisho ya demkrasia ya kweli kukamilika.
Matokeo ya uchaguzi huu, hayanishangazi na hayatanishangaza.
Uchaguzi wa 2015 haukuwa wa kuomba ridhaa ya Wananchi kuongoza Taifa bali ni kulazimisha wananchi wakubali mtawala fulani ili kuendelea kutawaliwa bila kuwa na ushirikishi.
Suala la Katiba mpya liligusiwa juu juu na vyama vikubwa kwenye uchaguzi (CCM/UKawa), halikupewa kipaumbele na ni wazi tunarudi pale pale tulipokuwa kabla ya uchaguzi wa 2010.
Kukosekana kwa msukumo wa kuweka kipaumbele kwa Katiba mpya, kumenufaisha CCM na Ukawa nikiwa na maana ya kuwa yeyote atakaye tangazwa mshindi, bado ataendelea kuwa mnufaika wa katiba mbovu, hatalipa kipaumbele kwa dhati na ile dhamira ya kujenga upya Taifa madhubuti itapotea.
Uchaguzi huu wa 2015 ulijaa vijembe vya ufisadi na tuhuma.
Zaidi umejaa mazingira ya kutokuaminiana hata kutokuamini vyombo vya dola (polisi, Usalama wa Taifa, Tume ya Uchaguzi) na hata taasisi binafsi (Twaweza nk).
Uchaguzi huu umejiendesha kwa ushabiki, hasira na dharau kwa wananchi na wa kulaumiwa ni sisi kundi tunalojiita "wasomi", "Wapembuzi", na wenye kutaka mabadiliko.
Pale vyama vikuu vilipoacha kufuata mkondo rasmi wa kikatiba na kanuni kupata wagombea wa Urais hata Ubunge na Udiwani, tulipaswa bila kujali tofauti za kiitikadi kusimama kidete kukemea dhambi hiyo kuu ambayo imekuwa ugonjwa sugu wa Tanzania.
Tutapiga kelele sana kuhusu Ufisadi, Rushwa na uadilifu, lakini kama sheria na katiba zilizopo hatuzitilii maanani hata kusimama wima kwa ukakamavu kuzilinda na kuzitetea, je katiba mpya tunayoililia itatusaidia nini ikiwa kwenye utekelezaji tunaendelea kupwaya?
Ni dhahiri tamaa ya madaraka ndio imekuwa taswira kuu ya uchaguzi huu. Demokrasia, Katiba na kanuni zimenajisiwa kwa sababu ambazo hazikuwa na mantiki hata kidogo na zimeonyesha madhaifu makubwa ya kiutendaji na maamuzi ya kinidhamu na kiuongozi ndani ya vyama vikuu.
Haijakaa akilini mwangu kuwa badala ya kufuata demokrasia na kanuni za kichama, Lowassa aliachiwa akachukua fomu kugombea, akapata udhamini takribani asilimia 20 ya wanachama wa CCM, bila kuhojiwa na kusulubiwa kupitia vikao yanayosemwa kuwa ni madhambi yake.
Najiuliza kama kweli Lowassa ni mhalifu na mtuhumiwa mkubwa kiasi hichi tunachoaminishwa, miaka yote ushahidi umepoteaje mpaka akahama chama na kukubaliwa na Tume ya Uchaguzi kuwa anafaa kugombea kuwa Rais wa nchi na zimebakia dakika chache kabla ya yeye kamari yake kuzaa au kudoda?
Ilikuwaje ndani ya CCM akalelewa na kumea kama gugu sugu na kuogopewa?
Je alipohamia Ukawa, ni kwa mantiki gani Ukawa walimuona sasa anafaa kushika hatamu baada ya kumtangaza kwa miaka nenda rudi kuwa ni fisadi? Zaidi ni jinsi gani "ushenga" ulifanyika kumleta Ukawa na hata kutegemea ataleta nguvu kubwa kwenye upinzani?
Sitaki kutumia muda mwingi kumzungumzia Lowassa hapa, bali naonyesha ni vipi uchaguzi huu ulivyokosa uadilifu (integrity) na jinsi sisi kama wananchi tunavyoburuzwa kwa maslahi na matakwa ya wenye kutaka kututawala.
Tanzania haitaweza kuwa na uongozi imara tunaoutaka kama Katiba na Sheria tulizonazo hazitafuatwa, zitadharauliwa na kupuuzwa na walio na mamlaka na madaraka.
Tulichokiona kwa ufanisi 2015 ni Watawala kuhakikisha uimara wa mamlaka na maamuzi yao bila kuhojiwa : cyber crime act, Statistics act, National Security Act, News Act, Gas Bill, na vijisheria vingine vingi ambavyo vinawalinda wao kama watawala na si sisi kama wananchi na hata katiba yetu.
Hivyo basi, tunarudi kwenye drawing board, na tutatumia miezi 12 ya kwanza kutambiana nan i mshindi, nani alisema nini huku tukijaribu "kuunda" serikali yetu ya kufikirika ya nani anafaa kuwa Waziri, Mkuu wa mkoa au balozi huku deni la Taifa linaendelea kukua, shilingi inaangamia, kero za wananchi za mahitaji ya kila siku: maji, chakula, afya, elimu, ajira, kipato na miundo mbinu vinaendelea na hamu yao ya kupata Katiba mpya ikiwekwa kando kutokana na "vipaumbele" vipya vya kujenga mishikamano na kutatua mifarakano ndani ya vyama na zaidi kujinufaisha posho na maslahi mapya yanayotokana na kodi zetu.
Wa kulaumiwa si Lowassa, si Kikwete, si Mbowe, si Mbatia, si Slaa, si Mkapa au hata Zitto, wa kulaumiwa ni wewe na mimi tuliokubali kujiingiza katika mchakato uliokosa tija na mwelekeo na kutumia muda kupeperushiana picha za umati wa nyomi, kushangilia koroga/zungusha, push up na vijembe vya kashfa, matusi, na takwimu za kupikwa.
Hongera kwa mshindi, umethibitisha kuwa Tanzania ni Kichwa cha Mwendawazimu au kama alivyosema Mkapa ni malofa na wapumbavu!
Kwa Kikwete, pumzika salama kwenye maisha ya Ustaafu, kazi uliyotumwa umeimaliza!