Ppf & mikopo

CHE GUEVARA-II

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2010
Posts
571
Reaction score
156
Wadau habari zenu?
Naombeni majibu ya maswali haya:

(1)Kuna bank yoyote au taasisi yoyote ya fedha ambayo inaweza kumkopesha mtu (mfanyakazi) kwa dhamana ya mchango wake wa PPF lkn akawa analipa deni la mkopo huo kwa kutumia mshahara wake? Kama ipo ni ipi, na utaratibu ukoje?

(2)Nilishawahi kusikia kuwa PPF inaweza kumkopesha mteja wake kupitia SACCOS.
Hiyo SACCOS ni yoyote ile au LAZIMA iwe imeundwa na wanachama tu? Na kama ni LAZIMA iundwe na wanachama tu ni LAZIMA wanachama wawe wanafanya kazi kampuni moja? Utaratibu wa kupata mkopo PPF kupitia SACCOS ukoje?

(3)Tukiachana na PPF na mikopo, inawezekana mtu kujiunga na SACCOS yoyote ile nchini (kwa maana ya kwamba si LAZIMA members wote wanaound SACCOS wawe wana-share something unique for them, mfano "wafanyakazi wa kampuni fulani tu"). Kama ipo ni ipi na iko wapi? Kwa Dar ipo na inaitwaje, iko wapi na utaratibu ukoje?

NATANGULIZA SHUKRANI!
 
Yani mkizungumzia fedha za ppf au nssf huwa roho inauma sana,fedha zetu hazitunufaishi sisi wafanyakazi bali zinawanufaisha wafanyabiashara wakubwa kina manji ambao hawachangii hata senti kumi kwa mwezi how come nina 5m mkashindwa kunikopesha hata 3m kwani si fedha zangu hata nikishindwa kulipa si zitabaki balance ya 2m? Lazima tupeleke malalamiko ssra wabunge kina mnyika,deo f,kangi nyoka wa shaba 2saidieni,hawa nssf na ppf wanatangaza wanatoa mikopo kupitia saccos ni changa la macho tu maana kuchukua saccos mkopo hauna tofauti na raia wa kitaa ambae hana balance nssf/ppf wote mnakaa miezi mi3.
~pili nssf/ppf ni wezi how come mtu alienza kuchangia let say 2004 mpaka 2006 labda akamake 4m hv 4m ya 2006 ni sawa na 4m ya 2013? Kwanin wasiwe wanafanya evaluation wakati m2 anataka kuchukua mafao yake?
 

King Kong III umenena ukweli!
Yaani ni wizi mtupu.
Mimi hapa nawazia tu ku-retire completely from being a slave (employed).
Kwa sababu kama hadi sasa at age 36 nina 40,000,000 Tshs PPF ninasubiri nini kuachana na utumwa?
Naona nikiendelea kuzubaa utumwani (in employment) itafikia kipindi niko at age 55 hizo 40,000,000 zimeshashuka thamani na kuwa na uwezo wa kununua ng'ombe mmoja tu!
Bado nawalia timing (najipanga mtaani through trial and error ktk the so-called "foolish business" by those they call themselves "walioenda shule" ili nijifunze changamoto zilizomo ktk hiyo foolish business nisije kukurupuka ku-retire kichwa kichwa halafu baadaye nikdondokea pua); nikisha-aanza kuweka mizizi nakata minyororo ya utumwa (najilipua)! 2017 iko mbali!
 
GEPF wana hiyo scheme mkuu. So far hiyo ndo nnayoijua kwa sasa.
Hao wengine sina hakika kama wana fanya hiyo (Labda kwa sababu sina info)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…