Premature maana yake mtoto amezaliwa kabla ya muda wake kufika, yaani kabla ya wiki ya 38-40.
Iwapo mtoto atazaliwa kabla ya wiki ya 35, mapafu yake huwa hayajakomaa kiasi cha kumudu maisha ya kawaida. Watoto wa namna hii hustahili kupewa huduma ya msaada ya kupumua ili waweze kuishi. Vilevile kabla hawajazaliwa mjamzito hutakiwa kuchomwa sindano ya kusaidia kukomaza mapafu mara tu zinapoonekana dalili za mtoto kuzaliwa premature au pale mjamzito anapokuwa na historia kama hii ya kujirudia premature.
Watoto premature wanakuwa katika mazingira hatari kwa sababu viungo vyao vinakuwa havijajiandaa kwa maisha ya nje. Kwahiyo ni lazima wawekwe chini ya uangalizi madhubuti wa wataalam mpaka inapothibitika kuwa wanaweza kumudu kunyonya na mifumo mingine kufanya kazi. Pia hatari ya damu kumwagika kwenye ubongo wao inahitajika kuzuiliwa kwa kuwapa vitamin K pamoja na kupima ubongokwa ultrasound.
Sababu kubwa inayosababisha watoto kuzaliwa premature huwa ni infection.
Mama mwenye historia kama hii anahitaji uangalizi wa karibu wa daktari bingwa wa wajawazito.
Poleni sana.