Dk Slaa ameeleza kila kitu kwenye kampeni zake kwamba pesa atazipata wapi.
Hata hivyo kwa ufupi tuu embu tafakari vyanzo hivi vya mapato vikidhibitiwa na ufanisi ukawepo.
1. Bandari ya Dar es Salaam.........Kuhudumia kwa ufanisi nchi za Uganda, Rwanda, Burund, DRC Congo, Zamba na Malawi.
2. Utalii.............. Uimarishe shirika letu la ndege halafu lilete watalii moja kwa moja toka ulaya, marekani, Uchina na kwengineko duniani.
3. Misitu................. Simamia magogo vizuri na usimamie pia uwindaji ili vitalu vitupe pesa ya maana.
4 Baraza kubwa la mawaziri........... Punguza mawaziri mpaka 15 au 20 maximum, utakuwa umepunguza L/Cruiser za 200m ngapi? mafuta, posho na gharama nyingine za kuhudumia wasaidizi wa mawaziri kama madereva, wafanyakazi wa ndani, nyumba, makatibu wakuu na manaibu wao, ofisi na vimada wao.
5. Ondoa ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya. ili uongeze mamlaka kwenye local goverment.
6. Dhibiti matumizi ya saerikali.......... Hakikisha mtu hapewi posho mara mbili kwa kikao kimoja,
7. Simamia vyema vyanzo vya mapato TRA, punguza kodi weka adhabu kali ili mtu aone kukwepa hakuna faida.
8. Bahari............ Hakikisha meli zote za kigeni zinazokuja kuvua samaki bila kibali zinathibitiwa. kama taifa, kesi kama ile iliyoko mahakamani maarufu kama kesi ya Magufuli inatakiwa ichukue siku kumi na nne tu hukumu kupatikana.
9 Hakikisha viwanda vya samaki vinawezeshwa ili samaki wasindikwe hapa hapa na kusafirishwa kama bidhaa na siyo mali ghafi.
10. Simamia vizuri utendaji wa halimashauri zetu, pesa zinazopelekwa hakikisha zinatumika kwenye miradi iliyokusudiwa, mkurugenzi mzembe aondolewe mara moja, wapewa KPI's na kishindwa anafukuzwa mara moja. Watanzania wenye uwezo wko kibao.
Haya ni machache, list ni ndefu sana kama unataka kuwa mkweli haya yako dhahiri, hayahitaji kuwa umeenda darasani kuelewa.
Respect.