Precision Air, Azam, UDSM, ITVna Clouds FM waongoza kwenyelist ya Super brands 2013

heaven on desert

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2013
Posts
1,025
Reaction score
393
Precision Air, Azam Products na
chuo kikuu cha Dar es Salaam
UDSM, ni miongoni mwa
makampuni bora 20 ya Tanzania
yaliyotajwa kama super brands kwa
mwaka 2013, kwa mujibu wa
kampuni ya utafiti ya jijini London,
The Centre for Brand Analysis
(TCBA).
Pia kwenye orodha hiyo kwa mujibu
wa TCBA, 2013/14 makampuni
mengine ni Vodacom, Mlimani City,
National Microfinance Bank (NMB),
Coca Cola na Fanta, na M-Pesa.
Mengine ni Kilimanjaro Drinking
Water, Chai Bora, Panadol, Foma
Gold, na Kilimanjaro Music
Award.Kwa upande wa vyombo vya
habari ITV na Cloud FM
vimeongoza.
 
Wangeweka na Vigezo walivyo tumia, Mfano kwenye Vyombo vya habari, Ni wasikilizaji na watazamaji au. Huu utafiti una walakini mwingi sana
 
Wangeweka na Vigezo walivyo tumia, Mfano kwenye Vyombo vya habari, Ni wasikilizaji na watazamaji au. Huu utafiti una walakini mwingi sana

zaidi ya hayo wangeweka na value za hizo superbrands na vigezo walivyotumia kukadiria hizo values.
 

udsm ni kampun au?
 
udsm ni kampun au?


Kasema brands; brand si lazima iwe kampuni. em fanya google ya neno brand uone inakupa maelezo yapi nadhani ni jina linalojenga haiba ya kitu; ambapo mwisho wake brand inakuwa kama jina la kusifika. Jina linaposifika (kwa mazuri of course) si lazima liwe jina la kampuni:laser:
 
Sasa Precision Air kwa lipi hasa lililowafanya wawe super brand? Kuchelewesha wateja uwanja wa ndege (delays and cancellations = disruptions)?
Au kuchaji nauli za juu sana kuwakomoa watanzania na kuifanya huduma ya usafiri wa anga kuonekana ni wa tabaka la watu wachache tu wenye nazo? Hili limethibitika baada ya ujio wa fastjet.
Nini hasa kilichoifanya PW kuwa super brand jamani mi sijaelewa. Lazima kuna vigezo ambavyo vimewekwa kushindanisha haya makampuni kwa kila category. Ningependa kujua walishindanishaje.
Muasisi wa uzi huu tafadhali njoo tena nikusome vizuri.
 

Swadakta mfano CHADEMA pia super brand.
 
Inatusaidia nini sisi wenyenchi
 
Chai bora??????????

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…