Nilipanda ndege yao toka Dar kwenda Mtwara (mwaka huu mwishoni), wakati tunaenda ingia kwa ndege tairi moja lilikuwa kama limebonyea, sasa kukawa na mjadala ni bovu ama vipi?, nadhani katika kujipa tumaini (ambayo ni hatari) mmoja wetu akasema ni kwa kuwa ina mzigo mzito. Tukapaa salama, tulipofika Mtwara, tukatua, lakini wakati ndege inageuza, ili iende kusimama, tukaona Moshi mzito, sasa pale kila mtu alikuwa kimya, manake hatukujua linaloendelea nje, labda ndege imeanza waka?, ama kuna nini?. Tuliposhuka tukakuta lile Tairi limepasuka na kutoa moshi vibaya mno, lilikaribia kuwaka. Nilichukua Picha, ila hiyo habari sikuioana kama ilitoka kwa vyombo vya habari. Huduma za ndege Tanzania kama hawatakuwa waangalifu, tunaelekea kuwa kama Congo (DRC).