Precision Air - Cancellations/Delays zimezidi

TheImporter

Member
Joined
Oct 13, 2011
Posts
23
Reaction score
2
Hii airline inaelekea kubaya esp. ukiangalia competition inayoingia nchini kwenye industry. Cancellations na delays zimezidi tena taarifa hazitolewi muda wa kutosha (say 3 or 4 hours) kabla ya safari ili watu wajue na kupangilia mambo yao vizuri. Kwa mfano leo, kuna ndege ambayo ilitakiwa kuondoka kwenda Mwanza saa 1210 jioni, nimefika airport wananiambia inataondoka saa 5 usiku. Kampuni haijali saizi haijali kabisa wateja tofauti na zamani, hawatowi taarifa mapema na hawaombi radhi. Ila abiria akichelewa anapigwa faini. Na kwa hili inaenda kupoteza wateja wengi wa kubwa.
 
Mkuu PakaJimmy, hii ndyo niliyosema kwenye ile thread nyingine!

Kwa nini isitokee basi angalau kwa WIKI MOJA tu, bila delay au kukatisha safari? Mkuu TheImporter pole, ninaungana na wewe kusema PW haiwajali wateja wake(kwa malalamiko yao, ushauri, hata kwa huduma mara wanapobadili ratiba kwa kuamua wao)

Inaudhi lakini hatuna namna ya kufanya!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…