Precision air kufilisika?

Precision air kufilisika?

Moony

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2011
Posts
1,599
Reaction score
436
Precision air inakabiliwa na madeni mengi na pia hailipi kodi ya mapato, na ilinunuaroute nyingi ambazo hawawezi kuzi service jinsi inavyotakiwa.

Ufisadi uliomo ndani ya kampuni ya Precision umekithiri na kama ATCL mu watu wa mikakati, hii ndo chance kwenu, changamkeni.
 
Wafilisike wakati hawana mshindani? Hujasikia wanavyokaribia kufaulu kumwondoa Fastjet kwa mbinu za ujanja baada ya kuimaliza ATC/ATCL?
 
Naomben muongozo mtu akitaka kuuya hisa zake katika kampun anafanyaje? mim nilinunua hisa kwenye hili shirika na ninataka kuuza help me with procedurez plz
 
Ukisikia wamefilisika ujue wadau wakubwa wametoa pesa zao na share zao wameziuza KQ na kwa Public...mwenyewe Michael Shirima amekaa pembeni anakunywa kahawa yake pale Kibo Palace taratibu!
 
Naomben muongozo mtu akitaka kuuya hisa zake katika kampun anafanyaje? mim nilinunua hisa kwenye hili shirika na ninataka kuuza help me with procedurez plz

Mh hata mie nilinunua hisa huko lkn kufilisika hapana!
 
Naomben muongozo mtu akitaka kuuya hisa zake katika kampun anafanyaje? mim nilinunua hisa kwenye hili shirika na ninataka kuuza help me with procedurez plz

jaribu kwenda kwenye soko la hisa watakuelekeza.
 
Wafilisike wakati hawana mshindani? Hujasikia wanavyokaribia kufaulu kumwondoa Fastjet kwa mbinu za ujanja baada ya kuimaliza ATC/ATCL?

Je ungependa kubadili mtazamo na maoni yako ?
 
Naomben muongozo mtu akitaka kuuya hisa zake katika kampun anafanyaje? mim nilinunua hisa kwenye hili shirika na ninataka kuuza help me with procedurez plz
Nenda ukiwa na hati yako ya hisa kwa mawakala wa soko la hisa kwa mfano Orbit Securities, nk - Ila kwa sasa usishangae wakichukua muda mrefu kuziuza, na pengine kwa bei ya hasara, kwa sababu ya hali ya mashaka ya precision.
 
Naomben muongozo mtu akitaka kuuya hisa zake katika kampun anafanyaje? mim nilinunua hisa kwenye hili shirika na ninataka kuuza help me with procedurez plz

mbona elimu huwa inatolewa hapohapo!unaponunua hisa! Na kuuza!
 
Naomben muongozo mtu akitaka kuuya hisa zake katika kampun anafanyaje? mim nilinunua hisa kwenye hili shirika na ninataka kuuza help me with procedurez plz

Mkuu waone DSE kwa utaratibu kamili koz kwa sasa mzigo ushakuwa listed pande hizo so they will give you proper guidance. Wanapatikana town tu hapo Jubilee Towers.
Pole kwa kuwa misguided mwanzo.
 
Wafilisike wakati hawana mshindani? Hujasikia wanavyokaribia kufaulu kumwondoa Fastjet kwa mbinu za ujanja baada ya kuimaliza ATC/ATCL?

Sina hakika kama data zako ni makini. Either way, wote makampuni ya ndege wana ushindani mkubwa na operating costs zilizo juu kwenye hiyo industry. PW kwa sasa hawana hali nzuri kwa kweli. Jamaa aliekuwepo pale zamani Alfonsi Kioko (AK) amefilisi kwa kiasi kikubwa sana. Ameliacha shirika lina madeni lukuki mpaka sasa more than 30 million USD wanadaiwa.
Wana mkakati wa kupunguza wafanyakazi na ndo wameanza na wafanyakazi walioingia na vyeti magumashi. Tayari washaanza kupigwa chini wengi tu mpaka sasa.
Wanajaribu kupursue cost cutting measures kwa kiasi kikubwa sana ili kupunguza bad spending.
At least I can laud Ms Sauda's efforts the newly appointed CEO from the same KQ.
 
Lisemwalo lipo kama halipo linakuja, wafanyakazi wao hawaonyeshi uchangamfu wao wa siku zote, juzi kwenye ndege yao moja walikuwa wanakosea hata matangazo. Halafu huduma zao za viburudisho imekuwa korosho na soda. Na juzi ndio ilikuwa biskuti mbili tu na maji au soda. Ukisema chai wananuna maana inabidi waanza kutazamana. Huduma hii ya refreshement inafanana hata kama ni muda wa jioni kabisa. Hii ni tofauti na walivyokuwa zamani na tofauti airline zingine. Jamaa anaweza kuwa na habari ya kufilisika kwao
 
Wako bankrupt,kuanzia juzi wamesitisha huduma zao Kigoma na inasemekana hazitarudishwa tena ''hadi notisi ya baba'' till further notice.inasemekana na kwingineko kwingi wamesitisha route.Mwenye macho aambiwi tazama,habari ni kweli kabisa.
 
Wamesitisha route ambazo hazina faida ili ku capitalize on the profit making routes.
Its a business strategy. You cut unnecessary costs for maximization of profits. Currently route zao za Mbeya, Mwanza na Kili ndo zinazowaingizia hela ndo maana wameongeza frequencies huko ili walau wapate faida itakayowawezesha kulipa madeni mengi yanayowakabili kwa sasa. Pili wameamua kurudisha maboeing yale coz running costs ni juu sana plus maintenance. Ukiwa na madeni halafu haupunguzi matumizi yako hamna tija unayoongeza kama unataka kuinusuru kampuni toka kwenye madeni.
 
Ukisikia wamefilisika ujue wadau wakubwa wametoa pesa zao na share zao wameziuza KQ na kwa Public...mwenyewe Michael Shirima amekaa pembeni anakunywa kahawa yake pale Kibo Palace taratibu!

unakumbuka hii?
 
Back
Top Bottom