Precision air maji shingoni

yahyaam

Member
Joined
Feb 13, 2013
Posts
18
Reaction score
3
Ndege za kamatwa na kushindwa kuruka madeni,kioko awakimbia awaacha katika hali taabani. Wafanyakazi walipwa nusu mshahara,waanza kupunguza route,wameshidwa kutoa huduma nafuu kwa wananchi. Wajaribu kuididimiza fastjet lakini wakwama,kiasi kwamba wadaiwa kila kona madeni yasiyo lipika. Wapo katika hatua ya kujikabidhi serikalini na walijaribu kuihujumu na kuisumbua air tanzania,hapo awali kwa mafanikio ya kutosha. Sasa wakwama kuihujumu fastjet na fastjet yaendelea kupaa kwakuwapatia watanzania huduma bora na zenye bei nafuu.
 
Habari haijatulia. Ndege zimekamatwa wapi? Wanadaiwa na nani? Ruti gani zimepunguzwa?
 
hata DAR Express kuna wakati walionekana kufulia na kasi ya Scandinavia ikionekana ingewamaliza kabisa lakini hadi sasa wanaendelea huku makampuni kibao yakiwa yamekufa. Wape moyo wajasiriamali na si kuwakatisha tamaa
 
hii story siielewi kama ambavyo sielewi ni kwa nini TANESCO wana record loss ilhali ni wenyewe wanao uza umeme tanzania! I cant understand.
 
Hii habari ni ya mtu aliyewahi fanywa kitu mbaya na Precision air..Ni ya kisasi zaidi
 
Kwanza
Boeing zimekamatwa,JNIA ziko grounded mpaka zilipe pesa nyingi tu. watoa huduma wote ikiwapo wakodisha ndege pamoja na huduma zingine na ndege nyingi zilisongiziwa kua mpya zote zinadaiwa na mabenki. Route nyingi zimeshasisitishwa Comoro inasuasua,kigoma chali,arusha bye bye.
 
Jeikei anaua nchi kampuni nyingi sasa zipo ICU zinaemea pua moja sio P.A nyingi tu zipo tahabani.
 
though i got your point lakini muheshimiwa hayo ni mabasi..hizi ni ndege..usichanganye madawa! mabasi na ndege ni vitu viwili tofauti!
 
Udaku spesheli
We sema tu udaku wakati wafanyakazi wanaangamia.. Una mtu yeyote unatemfahamu huko precision akupe uhakika? Kuna wengine kwa vile nyie hamna namna ya kupata taarifa mnaishia tu kusema huu ni udaku.. kalaghabhao
 
This is scary........wahaya tutaendaje bukoba bila plesisheni?
 
kuanzia lini?
 
Wapo katika hatua ya kujikabidhi serikalini na walijaribu kuihujumu na kuisumbua air tanzania,hapo awali kwa mafanikio ya kutosha. Sasa wakwama kuihujumu fastjet na fastjet yaendelea kupaa kwakuwapatia watanzania huduma bora na zenye bei nafuu.

Wakijikabidhi serikalini mbona ya ATC yatawapata! Hata hivi tangu lini mali ya watu binafsi wakajikabidhi serikalini? Au labda unazungumzia uwezekano wa kufilisiwa?
 
jamani Unajua precisionair ni moja kati ya MADE IN TANZANIA, inabidi tuhudhunike na si kufurahi, unajua fastjet ya nani? atleast ka prec kuna vishea shea vya watz nk angalau kuliko hiyo fast jet ambayo si yetu ingawaje ni kweli Prec wamekuwa na mijibei au campaign ya made in TZ tumeisahau? eti wajameni
 
Huyu mtoa mada ana mawazo ya kutawaliwa na wakoloni kwani Mtanzania Mzalendo anapofurahia kampuni ya kizalendo kufa kwa sababu ya kampuni ya kigeni lazima upstairs kuna hitaji rehab.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…