Precision air mbona kimya?

Precision air mbona kimya?

ram

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Posts
9,326
Reaction score
8,505
Jamani mimi nilikuwa mmoja wa watu walionunua hisa za Precision Air, nashangaa hadi leo ni kimya sijawahi kupigiwa simu wala kutangaziwa chochote thr media

Precision Air vipi au ni DECI no mbili?

Mwenye kujua kinachoendelea anijuze plz!
 
jamani hata mimi nina kilio hichohicho
 
sasa kama hawajapata faida gawio litatoka wapi?? crdb hisa ni sh 150 sasa hivi...kwa siku wanauza hisa kama 4-8 hahahhahahh njaa kali...
 
Tanzania na masoko ya hisa bado.... utafiti yakinifu hua haufanyiki na ukifanyika unakua doctored, na ukihoji huna nafasi
 
Precision haitafanya vizuri ,mngeuliza kwanza wajameni.poleni
 
Kuweni na subira jamani, kutoa dividend mpaka mwaka uishe wafunge mahesabu ndo wajue kama kuna chochote cha kuwagawia, kama hakipo basi ni kusubiri hata miaka5 inaweza pita. Kuwekeza kwenye hisa ni very high risk investment but sometimes it pays.
Kama vipi angalia share zikipanda bei pale DSE kauze uachane nao, ila kumbuka kuna commissions na kodi pia, so hakikisha bei imepanda hasa!
 
Tanzania na masoko ya hisa bado.... utafiti yakinifu hua haufanyiki na ukifanyika unakua doctored, na ukihoji huna nafasi

Hili ndiyo jibu sahihi kwa maoni yangu, Bongo yetu ukiwa na senti yako ya ziada bora uanzishe mradi hata wa maadazi kuliko kununua the so called HISA, bado tuna safari ndefu.
 
Unakumbuka TOL walianza lini kuuza hisa? Kama na wao bado hawajaweza kutoa gawiwo, basi idea ya kununua hisa kwangu inabaki na sifa ya 'extravagance'
 
Mi pia nilinunua hisa, shida yangu ni majibu ya hisa zetu na sio gawiwo, walisema january tutapata kimya mpaka leo kulikoni?
 
Mi pia nilinunua hisa, shida yangu ni majibu ya hisa zetu na sio gawiwo, walisema january tutapata kimya mpaka leo kulikoni?

Kwa yoyote alinunua shea, jee ulipewa hati ya umiliki kutoka Precision? Na kama hujapewa hati ya umiliki jee ni kitu gani walikupa kuonyesha kwamba wewe ni mmiliki wa kampuni?

Pili, gawiwo sio guarantee bali inategemeana na utetandaji (performance) ya kampuni. Sasa kama kampuni haijatengeneza pesa then msitegemee gawiwo?.

Wengi wanao nunua shea wanategemea gawiwo (dividend payout) lakini kuna vitu kama faida ya mauzo (capital gain) pindi utakapo amua kuuza share yako kwa faida. Kusema kweli biashara za watu kununua shea holela holela bila kujua au kuwa na ueleo wa soko la shea ni kitu hatari sana. Sababu wengi wenu mnategemea kwamba matokeo ya kununua shea zenu ni kupata faida.
 
Kampuni sio lazima itoe dividends hata kama imepata faida, ni maamuzi ya kampuni.
Apple walikuwa wana $100 BILLION in cash na hawakutoa dividend yoyote.
 
nyie mnao suburi sijui kupigiwa simu au kupewa gawio sikilizeni
na anza na wale wa simu-tangazo lilitoka juzi muende kwenye bank mlizo nunulia shares zenu mpewe cheti cha umiliki wa hisa ulizo nunua .

nyie wa gawio mme nunua shares juzi tu, mnataka faida leo faida ina weza take hata 1 year ndio mpewe ina tegemea na walivyo ingiza faida ila sana sana ni bada ya 1 year ndio mtaona matunda yenu
 
Kitu chakuwekeza bila kupata hasara ni ardhi.Hata kama unapesa kidogo nenda sehemu yeyote Tanzania nunua ardhi kuliko kuwekeza pesa ambazo zitaliwa na uongozi wa kampuni na wajumbe wa bodi.Ardhi haimtupi mtu,period
 
Tanzania na masoko ya hisa bado.... utafiti yakinifu hua haufanyiki na ukifanyika unakua doctored, na ukihoji huna nafasi

Ni ukweli mchungu sana huu. Usinikumbushe NICOL na Tanzania Oxygen Limited

Hili ndiyo jibu sahihi kwa maoni yangu, Bongo yetu ukiwa na senti yako ya ziada bora uanzishe mradi hata wa maadazi kuliko kununua the so called HISA, bado tuna safari ndefu.

Sure. Ni bora ukawekeza katika ardhi ama biashara nyingine, lakini hisa za Tz zina mizengwe sana. Kidooooogo TBL na Sigara angalau wanatoa gawio, lakini wengine ni maumivu kwa kwenda mbele
 
Back
Top Bottom