Haya ndiyo mambo ya kufuatilia kwa kampuni makini.Precission ni kimeo kwa kweli kuna jamaa mmoja pale mwanza anaitwa Dismass anakera sana...
usije ambiwa uende kumuona ni mzinguaji ile mbaya.....
Mkuu sasa hapo wanafungaje mkanda??Hawana mana hawa PW tena kama unakwenda kwenye mkutano watakuchelewesha ujute,kuwapa watu seat 1 watu wawili ndio zao....
Hivi kweli jamani route ya humu ndani ya nchi from Mwanza to Dar ndege inatua Dar saa tisa usiku? Hii ni ile yenye ratiba inayoonesha inaondoka saa kumi na moja!
Kwanza mna customer care mbovu, hamjali kabisa wateja, mnawatreat mnavotaka nyie!
Sikilizeni; kama msharidhika kaeni pembeni tujikongoje na Air Tanzania yetu! Mnatukera sana sio siri, hapo ni hivi vindege viwili; mkiwa na dozen si ndio itakua issue?
Mmbongo akipata bwana aaahaaagahhhhhh mmm******$$$##
Ntaendelea kupanda mabasi yangu kuliko kufika usiku saa sita.
Mkuu ni kweli kabisa!
Mimi sijawahi ona ndege abiria wanazidi! Siku moja tulikua tunatokea Kilimanjaro kupitia Znz, ndege ilikuwa imeshajaa ili hali kuna abiria kutoka Zanzibar kwenda Dar. Wakapanda abiria wanne; hakuna seat, wakagoma kushuka! Ilikua kizungu mkuti, ikabidi sie abiria ndio tuwabembeleze manake walishasema hawashuki, wameshachelewa sana; na ilikuwaje wasijue kuwa ndege iko full? Kichekesho kitupu!
Precission ni kimeo kwa kweli kuna jamaa mmoja pale mwanza anaitwa Dismass anakera sana...
usije ambiwa uende kumuona ni mzinguaji ile mbaya.....
Imeshanitokea;
JRO-DAR! Ndege ya saa 7 mchana ikabadilishwa kuwa saa 1 jioni; mara napigiwa simu "ndege yako imebadilishwa utaondoka saa 3 usiku; Kufika JRO Airport mnatangaziwa kuwa "kutakuwa na ucheleweshwaji kidogo" mnaondoka saa 5 usiku!!!
Sasa wewe ni mgeni A town, chumba cha hoteli umesha-check out tangu asubuhi, inakuwa shida unabaki kuzurura madukani. What a shame!
Kweli ni bora ATCL kwani kwa ndege yao moja tu, safari za Kigoma/Tabora hazina mizengwe hii!