Precision Air wawajibike kwa kuwachelewesha abiria 'airport' bila maelezo yanayoeleweka, "tumekaa zaidi ya masaa matatu"
Abiria ambao tulikuwa na tiketi za kusafiri na ndege ya Precision Air kutoka Dar es Salaam - Arusha, Oktoba 14, 2024, Saa 12 Asubuhi tumeshindwa kuondoka kwa wakati na wahusika hawatoi maelezo yoyote kwetu yanayoeleweka kuhusu changamoto hiyo.
Abiria tumekaa tu hatuelewi nini kinaendelea, wengine tulikuwa tunawahi kwenye majukumu, lakini kibaya zaidi ambacho sio jambo rafiki kwa Kampuni kama hiyo ni kwamba wahusika hawakutueleza kwa wakati kama kuna changamoto zaidi ya saa tatu.
Baadaye wanaanza kutufaulisha bila utaratibu wowote na abiria wengine wamepandishwa ndege zisizoendana na hadhi ya tiketi zao, lakini cha kusikitisha zaidi ndege ambazo wengine tumepandishwa zinapita route tofauti mpaka kufika Arusha.
Kwa kweli jambo hili ni kero siwezi kulikalia kimya, naamini zipo mamlaka ambazo zinatetea na kulinda haki za abiria kama ilivyo kwao ukichelewa kidogo huna chako lakini wao wanaenda kinyume na makubaliano kupitia tiketi hata kutoa maelezo yanayoeleweka wanashindwa, sijui kama hata kumekuwepo na uwajibikaji kwa mamlaka kuwachukulia hatua kampuni zenye changamoto hizo.
Wito wangu kwa mamlaka naomba wafuatilie kwa ukaribu kero hiyo, inapobainika uzembe kampuni husika ziwajibike kama abiria anavyowajibika inapotokea changamoto ambayo ameisababisha yeye hususani kuchelewa, tukikalia kimya suala hili tunakuza na kubariki uzembe.