Prediction: Afisa Aliyatuma Vijana kufanya Uovu Hatoguswa

SankaraBoukaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2019
Posts
1,213
Reaction score
1,918
Afisa wa jeshi, kama mtu mwingine yeyote mwenye mamlaka, anaweza kutumia vibaya mamlaka yake au mamlaka yake juu ya raia. Matumizi mabaya kama hayo yanaweza kuchukua aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vurugu za kimwili, unyanyasaji, kulazimisha, au aina nyingine yoyote ya ukatili ambao unakiuka haki na hadhi ya raia.

Ni muhimu kutambua kuwa wanajeshi kwa kawaida hufuata kanuni kali za maadili na sheria, ndani ya jeshi na kuhusiana na raia. Matumizi mabaya ya mamlaka na maafisa wa jeshi kwa kawaida huchukuliwa kuwa makosa makubwa na yanaweza kusababisha hatua za kinidhamu, matokeo ya kisheria, na kuharibu kazi zao.

Iwapo afisa wa jeshi atatuhumiwa kutumia vibaya mamlaka dhidi ya raia, tukio hilo kwa kawaida huchunguzwa na mamlaka husika, na afisa huyo anaweza kukabiliana na matokeo ikiwa atapatikana na hatia.

Katika nchi nyingi, kuna mifumo ya kisheria ambayo inalinda raia dhidi ya matumizi mabaya ya wanajeshi na kuhakikisha uwajibikaji.

Pia soma >
Polisi yaanza kufuatilia tukio la Binti aliyebakwa mande na wanaume watatu
 
Angekua mkubwa kuliko Amiri Jeshi mkuu asingekamatwa. Kwa vile sisi sote ni wadogo kwake sheria lazima ifate mkondo
 
Afisa wa jeshi, kama mtu mwingine yeyote mwenye mamlaka, anaweza kutumia vibaya mamlaka yake au mamlaka yake juu ya raia. Matumizi mabaya kama hayo yanaweza kuchukua aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vurugu za kimwili, unyanyasaji, kulazimisha, au aina nyingine yoyote ya ukatili ambao unakiuka haki na hadhi ya raia.

Ni muhimu kutambua kuwa wanajeshi kwa kawaida hufuata kanuni kali za maadili na sheria, ndani ya jeshi na kuhusiana na raia. Matumizi mabaya ya mamlaka na maafisa wa jeshi kwa kawaida huchukuliwa kuwa makosa makubwa na yanaweza kusababisha hatua za kinidhamu, matokeo ya kisheria, na kuharibu kazi zao.
Iwapo afisa wa jeshi atatuhumiwa kutumia vibaya mamlaka dhidi ya raia, tukio hilo kwa kawaida huchunguzwa na mamlaka husika, na afisa huyo anaweza kukabiliana na matokeo ikiwa atapatikana na hatia.

Katika nchi nyingi, kuna mifumo ya kisheria ambayo inalinda raia dhidi ya matumizi mabaya ya wanajeshi na kuhakikisha uwajibikaji.
Wale vijana watakamatwa,
kutakuwepo na ubabaishaji mwingi, siku, miezi miaka itapita.
Mpaka watu wasahau.
HAKUNA KITAKACHOTOKEA KWA WABAKAJI.
 
Hata kama walitumwa Hilo jumba bovu ni lao maana si ndio walikua wanasikia utamu basi inabidi wagharamie ule utamu waliokua wanaupata afande mkuu namtetea asihusishwe maana unakubalije kutumwa ukafanye kitu kama hicho na ujirekodi na misula kabisa
 
Huo ndio ukweli.Na Kwa taarifa za kuaminika huyo aliyetuma amelindwa na jeshi.polisi wameambiwa tokeni hapa tutamshughulikia wenyewe.
 
Jeshi letu tunalolipa sifa kedekede mpaka muda huu halijatoa taarifa kwa kina kueleza umma nini kinaendelea?
Hapa nchini kwetu kuna watu wako juu ya sheria, mfano watu wa Tishii na jeiwii wengine ni wabunge hata wakikosea kesi itamalizwa kiaina.
 
Vipi kuhusu Gekul aliyeagiza kijana aingiziwe chupa kwenye makalio? Aliishia kutumbuliwa tu! Hata huyo RC ataachiwa tu ukiwa kada wa chama uko Immune huwezi kufungwa maisha

Wanaachiwa kwa kucheza na loophole za kikatiba(kisheria).....Tukipata wanasheria wazuri kama kina Mwabukusi na Kibatala aachiwi mtu.
 
Angalau hawa waliofanya tukio inabidi sheria ionyeshe makali yake, ni jambo baya sana linaloharibu image ya nchi.
Sheria gani inabagua? Ukimtukana kiongozi unakamatwa ndani ya dk 5 ,mwananchi akitekwa /kulawitiwa polisi wanachunguza. Hiyo video haina haja ya kuchunguza.

CO angepaswa kuwapeleka mahakama ya jeshi wafukuzwe then wakabidhiwe uraiani
 
Na
Hata kama walitumwa Hilo jumba bovu ni lao maana si ndio walikua wanasikia utamu basi inabidi wagharamie ule utamu waliokua wanaupata afande mkuu namtetea asihusishwe maana unakubalije kutumwa ukafanye kitu kama hicho na ujirekodi na misula kabisa
Naye kashiriki, kuna video moja binti kaambiwa aombe msamaha kwa afande!! Ni mhusika namba moja
 
Back
Top Bottom