Boss, 1ZZ hakuna ya cc1750 bwana. Zipo za cc1794 na cc1796, ambazo zote zinafupishwaga 1.8L tu.
Hiyo ZZ-FE ya kwenye Premio 1st gen ni cc1794, ni moja ya engine maarufu na imara iliowahi tengenezwa na Mjapan. Kwanza ipo kwenye magari mengi sana mfano Corolla, Rav 4, Opa, Wish, Avensis, Isis, Alion etc etc.
Kwa maana hiyo usiogope kabisa kuhusu spare parts za engine, kwa hapa mjini.
Premio ya 2nd generation zilianza mwaka 2007, sasa wewe unayosema 2005 hiyo ni 1st gen.
Tuanzie hapa, unaweza sema exactly mwaka wa hiyo gari coz 2nd generation walitumia 2ZR-FE engine.