Presha na mihemko imeisha, njoo tuijadili Derby kitaalam

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Hatimaye tarehe 23/10/2022 ikafika baada ya siku kadhaa za tambo, ngebe na kelele nyingi kutoka kila upande. Kwangu Derby ya safari hii ilitawaliwa na saikolojia ya nje ya uwanja kati ya wale wa sizitaki mbichi hizi na wale wa kuendeleza rekodi kwanza ya kumfunga mtani na pili kuendelea kuwa 'Unbeaten'.

NDANI YA UWANJA
1. Wachezaji wa kila upande waliingia na hofu na tahadhari kubwa hasa upande wa Simba. Ile Simba tuliyoizoea ikicheza kwa ku flow kupitia beki za pembeni ikawa tofauti kidogo. Zimbwe na Mwenda walichukua tahadhari kwani Nabi aliwawekea Tuisila na Moloko, hii ikawafanya wasipande juu ovyo. Simba walikuwa hatari sana kwenye counter attacks na km Okra angeacha ubinafsi na uchoyo kuna nafasi km mbili hivi huenda zingebadilika kuwa magoli.

2. Tuisila na Moloko wajitathimini kama kweli wametoka nje kuja kuongeza thamani kwenye ligi yetu. Wanacheza staili ya mawinga wa kizamani. Kwenye soka la kisasa winga huwezi tegemea mbio tu. Wao kila mpira ni kukimbia halafu si wazuri kwenye kukaba pindi timu ikiwa haina mpira. Angalau Moloko anauafadhari tatizo ni kubwa mno kwa Tuisila. Tuisila hana uwezo mzuri wa kumiliki mpira,kupiga chenga na hata krosi zake nyingi hazina macho.

3. Mayele anachakujifunza kutoka kwa Phiri. Siyo kila mechi lazima afunge yeye ana ubinafsi sana ndiyo maana ana takwimu chache za usaidizi. Jana licha ya kukabwa sana na Onyango na Inonga bado alipata nafasi kadhaa ambazo kama angeweza kutoa pasi kwa wenzake angeweza kuisadia timu zaidi.

4. Okra jana angeweza kuwa shujaa ila uchoyo umeikosesha timu yake magoli zaidi. Kwa zile nafasi alizozipata kama angetoa pasi kama Chama alivyofanya kwake basi kuna magoli yangeongezeka. Alizingua sana licha ya kufungia timu yake goli pekee.

5. Yanga inabidi watafute kiungo mkabaji mwenye kasi zaidi ya Aucho. Faulo nyingi alizocheza Aucho ni matokeo ya kuzidiwa mbio na kupelekea kuchelewa kuufikia mpira kwa wakati.

6. Ki Aziz, Licha ya kufunga goli bora la viwango vya duniani bado namuona hajafikia kiwango km alipokuwa Mimosa. Nilimuona akipoteza mipira kadhaa, papatu papatu nyingi na ni mzito kidogo. Kocha wa mazoezi amfuatilie zaidi. Pia Mipira ya kona inamsumbua kupiga, kona zake nyingi hazifiki zinakuwa fupi zinaishia kwa mabeki. Pamoja na mapungufu yake bado ni mchezaji muhimu.

7. Hali ya joto iliathiri mchezo. Kuna muda hasa kipindi cha kwanza niliona wachezaji wakijimwagia maji mara kwa mara kutokana na joto kali.

8. Refa alijitahidi kwa kiasi chake japo sikuona sababu ya kubwatukiana na wachezaji mara kwa mara huku akitoa mimacho kama nini sijui!

Yote kwa yote mchezo ulikuwa 50 x 50, na kila timu imepata ilichostahili.

Nawasilisha.
 
Tuisila alikua anazurula tu yule sio mchezaji wa kufanya Kambole aachwe.
 
Farid musa alitakiwa aanze mechi ya jana na sakho hakutakiwa kuanza hana faida kwa team isipokuwa na mpira halafu anatolewa anauliza vipi simba walitakiwa wamalize game mapema Jana kama habibu kyombo angeanza basi story ingekuwa tofauti leo.
 
Ukweli ni kwamba mchezo wa jana ndiyo mchezo uliokuwa raisi zaidi kwa simba kushinda kutokana na yanga kuelekeza nguvu na akili zao kwa club Africa.

Jana yanga hawakucheza kabisa mpira wao ule wa pasi nyingi,kasi ya 5G na mbinu za maangamizi.

Yote kwa yote, Yanga inapotea sana kwenye counter attack. Mechi ya 3 mfululizo anafungwa kwa counter attack.
 
Bila kusahau kituko Cha Jana, Mchezaji (Okrah) kushangilia kwa kuvua Jezi Dakika za mapema isiivyo kawaida (Dk. 15).

As If goli lake limemaliza mechi na wameshinda.

Amei-Cost timu Jana imeadhibiwa kwa kuwa na jumla ya Kadi 5 za njano ktk mechi Moja.
 
Ni mchezaji mzuri lakini anaonyesha hajafit bado kuwa mchezaji wa Simba SC, kwanza kaonyesha ubinafsi wa hali ya juu kitu ambacho kinatarajiwa kufanywa na wachezaji wadogo wanaohitaji ku prove something katika jamii ya wapenda mpira, angeweza kusababisha Simba kushinda goli 3 hadi nne kama angekua team player. Nafikiri anahitajika sasa apumzishwe hadi pale atakapoweza kucheza kama team. Speaking of winning Simba fans hearts, hutakiwi hata kufunga magoli manne kwenye game moja, wezesha timu ishinde utapendwa utakumbukwa, ajifunze kwa kina Kichuya, Singano, miquisone, Chama, Okwi na wengine, tunawakumbuka sana sio kwasababu wanamagoli mia ya Derby, hapana ila kwa nafasi yao waliweza kuisaidia team kushinda. Ningekua Mgunda angechezea benchi hadi ajifunze.
 
We Mikia FC tupu.
 
Jana kila timu imepata inachostahili...ndio uhalisia wa hali za timu zetu pendwa.
 

Kwa hiyo yanga akielekeza akili simba haelekezi klabu bingwa??we jamaa bhn
 
Ukweli ni kwamba mchezo wa jana ndiyo mchezo uliokuwa raisi zaidi kwa simba kushinda kutokana na yanga kuelekeza nguvu na akili zao kwa club Africa.
Tangu lini Yanga wakaelekeza nguvu kwenye mchezo wa kimataifa mbele ya mchezo dhidi ya Simba?
 
Mechi kama zile za ushindani wa 50/50 huwa zinaamuliwa na uzoefu binafsi, ni pasi ya Chama ndio iliamua goli kwa Simba na Shuti la Aziz Ki ndio liliipa Yanga goli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…