Niliwahi kusema hapa kwamba wanaomshauri raisi na kumuandikia Hotuba walikuwa wanaboa, kwa kuwa hawakuwa hata wana-capture issues muhimu na kumfanya Raisi aongelee vuvumi na mambo ambayo mengine hayakupaswa kuzungumziwa na nafasi ya Uraisi. Niliongelea pia jinsi raisi anavyopresent ilivyokuwa inaboa.
Lets be realistic, tuache ushabiki wa kijinga, no matter how bad we felt about our president, binafsi niko so impressed na setup ya hotuba ya leo (Ya Mwisho wa Mwezi wa July 2012), from the audience aliyoihutubia mpaka jinsi alivyokuwa anazungumza. Ni tofauti na wakati mwingine maana kuna wakati nilifeel ni puppet inaongea it was o boring yeye kuongea na screen na si kuongea na watu. Well done Washauri wa kipindi hiki na well done president for thinking out of the Box. You have skipped so many unnecessary critiques. I even enjoyed the way you present your issues, in a very presentable meeting the language and expression of many. Nimefurahi sana jinsi ulivyokuwa unachambua ishu umeonekana hujakariri unajua unachoongea hasa na unavutia kama Raisi. Nawachukia waliokuwa wanakupotosha.
Hapa anaonyesha yeye siyo Raisi wa CCM kuongea na Wazee wa CCM ambao mda mwingi wanasinzia anapokuwa wanahutubia hotuba yake ya Masaa 3, na kuongea na Screen akiwa ameganda utadhani amekariri akiwa anateswa na taa za studio huku wakati mwingine machozi yakitaka kumtoka, ukizingatia na suti hadi jasho linakuwa linamtoka.
Hon President never go back to that situation.
@Profesa, binafsi yangu usanii huu hata siku moja hauwezi kunivutia....Waswahili tunasema anayelia sana msibani huwa ndio mchawi..Binafsi sikuridhika na hotuba hiyo kwa sababu ni acting nzuri sana kushinda Oscar ya sinema, kitendo cha kuonyesha mtu akilia ndani ya suti kali na ya gharama..Hotuba haiko realistic ni mazingaombwe tu.. Kilichofanyika hapa ni reaction as to disaster recovery! hakuna zaidi ya kilio cha mchawi kurudisha imani za watu kwamba sii yeye mchawi bali kazi ya Mungu..Kama serikali ingekuwa imejiandaa vya kutoisha na swala hili limetokea tungesema well sababu ni hii lakini hizi sababu zimeanza toka Meli ya MV Bukoba na zinaendelea hadi kesho..
Ukitazama ajali ya Meli zilizotokea Zanzibar haiwezi kuwa ndio Uamasho kwetu ya kufikia makubaliano ya sheria na taratibu wakati hata Bara Meli zilisha zama na wala sii moja. Hivyo tunapokubaliana kuwa na sheria moja ina maana gani kusaidia ajali ikiwa hata bara sheria zipo isipookuwa zinakiukwa siku baada ya siku na kila inapotokea ajali tunamsingizia Mungu..The fact ni kwamba tumeshindwa kabisa kuondoa UHABA wa vitu nchini toka majumbani, ajira, maisha, shule, Hospital, Usafiri na hata nguo nadio maana tunavaa mitumba zaidi.. Na maadam kila ktu tunategemea kuagiza nje Uhaba huu hautakwisha na hizo sheria zitabakia vitabuni kwa sababu hakuna nchi inayoweza kutumia sheria palipo na UHABA (Scarsity)..Uhaba ndio chanzo cha Corruption na kama hakuna vita ya corruption, sheria haiwezi kuwapa kinga wananchi..
Ebu tazama ajali za barabarani.. umewahi kumsikia rais akizungumzia? Je unajua ya kwamba mwaka jana tu wamekuwa zaidi ya watu 20,000 na mwaka uliopita.. tuseme ktk miaka sita iliyopita wamekufa watu zaidi ya 100,000 kwa ajali za barabarani tu..Tumeshindwa kutazama ubora wa Daladala, Mabus, Malorry, Meli, reli yaani kote huko yanaua watu kila siku, tumeshindwa kusimamisha sheria kwa vitu tunavyokutana navyo kila siku barabarani itakuwa meli baharini?..itawezekana vipi swala la meli naa usafiri wa majini wakati tuna shida kubwa ya vyombo hivi vya usafiri.. Watu wataendelea kubeba abiria zaidi ya idadi na tutaendelea kutumia sheria mbovu kwa sababu tumeshindwa kukidhi Uhaba uliopo.
Swala ma Mafuta na gas:-
Watanzania hawataki kujua habari za visima vingapi vinachimbwa bali rais anawahakikishia wananchi ni kiasi gani cha asilimia serikali yetu inamiliki au itamiliki ktk visima vilivyokwisha patikana na kutoa gas. Na binafsi yangu hadi kesho sintokubaliana na wazo la kuvuta gas Dar ati kwa sababu ya ahadi ya kuzalisha megawatts 3,500 ambaoz zinategemewa kupatikana kufikia mwaka 2015..Huu ni usanii mwingine kabisa na kwanza hizo 3,500 ni total megawatts tunazozitegemea kutoka uzalishaji wa aina zote sio gas tu.. Hizi sasa tuna megawatts 350 ktk gridi ya taifa hizi zote ni za dharura ambazo hatuwezi kujivunia.. Sasa tunapeleka Bomba Dar ili kulishwa vyombo gani?.. Tanesco wameisha agiza mitambo ya kuzalisha umeme ya mega watts ngapi hadi tulete bomba la gas Dar?..Halafu huwezi kutumia gas sehemu moja maana kusafirisha umeme ndo ghali zaidi. Kwa nini wasianze na kuzalisha Umeme huko huko Mtwara, Lindi na Pwani na kama kunatalkiwa bomba la kuja Dar basi litoke Pwani kwa sababu ni karibu na litaweza kuzalisha umeme kwa ajili ya Dar..
Kama kweli tunataka kuzalisha Umeme wa gas Dar basi hii haitakuwa na maana yoyote kwa mikoa ya Mbeya Sumbawanga, Iringa hadi Kigoma na Tabora kwa sababu tutaendelea kusafirisha Umeme na sio gas kutoka Dar kwenda maeneo hayo kwa kupitia gridi ya Taifa. Hatuta save cost zozote. Kinachotakiwa kufanywa ni kuweka mipango sawa, wazi na cheap kwa watumiaji.
Matumizi gas majumba ya watu:-
Ni kweli Gas ilitumiwa sana na nchi za magharibi ktk mageuzi ya kiuchumi toka miaka ya 30 hadi 60 lakini miji mingi hawatumii tena gas majumbani kutokana na hatari zake, hivyo nyumba nyingi za kisasa wanatumia majiko ya Umeme badala ya gas kwenda moja kwa moja majumbani. Kweli gas ni rahisi Cheap lakini p[ia ni hatari sana..
Sasa nambie ikiwa Ulaya wenye utamaduni wa maintanace wanaihofia gas majumbani itakuwaje sisi Wadanganyika ambao hata bomba la maji tu tunashindwa kuli maintain?. Je, watakufa wangapi hali hata zima moto yenyewe shida...Moto wa gas tunaujua? huu ukianza nyumba moja utafuata bomba hadi bomba na pasipo immidiate respond unaweza kuondoa mji mzima. Sisi tumejiandaa vipi? kwa nini tusiendelee kutumia gas za mitungi ambazo ni safe zaidi kuliko kuweka mabomba ya gas ambayo walalahoi wanaweza kuyang'oa wakifikiria biashara ya chuma cha shaba?. Kosa la mtu mmoja au nyumba moja kusababisha vifo wa mamillioni ya watu?..
Nitaendelea.....