President Trump has been Impeached after the House of Representatives voted in favour of charging him with abuse of power and obstruction of Congress

MKUU Mpaka ukiwa impeach ujue ushahidi upo....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Democrats wanahitaji watu 67 kushinda Senate Trial. Wao wako 45, Independents wako 2 Republicans 53. Hivyo wanahitaji jumla ya Republicans 20

Sent using Jamii Forums mobile app
Bila kusahau there was no pressure, no threatening no quid pro quo: hayo yote yapo kwenye transcript ya voice call na hata raisi wa ukraini kakiri mara mbili kulikuwa hakuna hovyo vitu, Trump yupo innocent, hii impeachment ambayo imegeuka kituko itamuongezea trump na republicans pints kibao, Anyway Democrats walishasema wata impeach kwa namna yoyote ile hata kama ushahidi haupo na matokeo yake walivyo harakisha haya mambo jana wamepata aibu kubwa sana walippona kesi haina mashiko (weka case) kitu kilichopelekea kuomba kuongeza witnesses, mtu mzima mitch akawaambia mnavuna mlichopanda senate sio sehemu ya kufanyia homework za kazi zilizofanywa kwa uharaka bila umakini......Trump kashindikana
 
POST HII ILIUNGANISHA POST MBILI TOFAUTI NA ILIPAA MTANDANONI BILA IDHINI YANGU KWANI NILIKUWA SIJAMALIZA KUZIANDIKA. NITAANGALIA HIYO TABLET NILIYOTUMIA KUZIANDIKA. KWA VILE IMESHAPAA; NITATAFUTA MUDA KUZIEDIT POST ZOTE MBILI KWA PAMOJA BAADAYE

Kichuguu
Samahani Mkuu, hili suala LA impeachment naliona lakini sijapata muda was kulifuatilia kwa undani. Naomba kama unafahafu ueleze kwa undani na kwa lugha rahisi makosa ya Trump no yapi hasa?
Kuna mambo matatu yanayoshirikiana kumfanya Trump aonekane kuwa na hatia:

(a) Hali ya Rushwa Ukraine: Ukraine ni taifa ambalo lilikuwa na rushwa sana hasa wakati wa utawala wa zamani wa Yanukovych na hata utawala uliofuatia wa Poroshenko. Hata hivyo wakati wa utawala wa Poroshenko mambo ya rushwa yalipungua kidogo ingawa hata Poroshenk alikamatwa kwenye skendo ya rushwa kupitia Panama papers. Ndipo huyu kijana Zelensky alipopiga kampeini mkiuwa atapambana kusafisha rushwa na akashinda uchaguzi. Sasa hapo kuna mambo mawili matatu yanayoigusa Marekani kisiasa:
(i) Mykola Zlochevsky alieywahi kuwa Waziri wa Mazingira na mali ya asili wa Ukraine chini ya utawala wa Poloshenko alianzisha kampuni iliyokuwa ya gesi inayojulikana kama Burisma akairegister Cyprus . Bwana huyu akatuhumuiwa kwa makosa ya kutakatisha fedha, na kukwepa kodi. Kwa hiyo mwendesha mashtaka mkuu wa

(i) Wakati wa utawala wa Obama serikali ya Ukraine iilibanwa sana na mataifa yote ya Magaribi ikiwa ni pampoja na IMF na World bank kuhusu hali ya rushwa; wakati huo Biden ndiye aliyekuwa amepewa portfolio la Ukraine. Mataifa hayo ya Magaribi yakaona kuwa Mwendesha mashataka mkuu wa nchi alikuwa naye ni mtu wa rushwa alikuwa hawashughulikii watu wenye tuhuma za rushwa, hivyo wakaweka pressure afukuzwe kazi, na kweli akafukuzwa kazi.
(ii)


Bunge la Marekani lilidhidisha dola milioni 390 kuisaidia Ukraine kijeshi ili iweze kupambana na uvamizi unaotokea Urusi. Lakini yeye kabla ya kuzikabidhi fedha hizo huko Wizara ya mambo ya nje ili zipelekwe zilikolengwa, akazibana akimtaka rais mpya wa Ukraine atangaze kuwa atafanya Uchunguzi dhidi ya Biden kwa vile mtoto wa Biden aliwahi kuwa na kazi kwenye shirika moja la nishati huko Ukaine akawa analiwapwa dola milioni 50 kwa mwezi wakati Biden akiwa ni Makamu wa wa Rais.
Wewe ndiyo hujui mzee wangu; sijui huwa unapata wapi taarifa zako. Inawezekana uasoma magazeti ya Braitbart, au unasikiliza habari za Tucker Carlso,m au Sean Hannity na wana habari wa namna hiyo. Lakini iwapo unasoma habari za mazaeti yenwe journlaists professionals kama Wall Street, Wahsington Post, New York Times usingesema hivyo. Kuhusu PornStar - Kuna individual number 1 bado kesi imewekwa pending mahakamani, hiyo ni kes iko SDNY ambapo Michael Cohen leo yuko gerezani. Kuhusu Russia Collusion, ni wazi kuwa hukusoma ripoti kwani ilisema kabisa kuwa Campaign ya Trump ilipokea msaada wa urusi ili kusubotage campain ya Clinton, lakini uchunguzi haukuweza kupata ushahidi wa kutosha kuhusu Conspiracy. Elewa kuwa Collusion siyo kosa la kisheria bali kosa ni Conspiracy na ushahdi wa conspiracy inahitaji kutoka pande zote mbili za conspiracy. Kutopatikana kwa ushahidi wa kutosha haina maana kuwa hakuna ushahid, ni kwamba upo lakini siyo wa kutosha kwa maana kuwa huenda mashahidi wengine hawako tayari kutoa ushahidi au hawapatikani, kwa mfano Trump mwenyewe alikataa kuhojiwa, halafu yule Natalia Veselnitskaya hakupatikana kuhojiwa kwa vile alsiharudi urusi, na wale warusi wengine walikuwa indicted hapataiknai kwa vile wako urusi. Elewa pia kuwa swala ya Russion Collusion halikuwa la Democrat bali lilikuwa la FBI na lilikuwa limeanza hata kabla hajawa rais. Mwisho, hii ya Ukraine ushahidi umetolewa na watu walioajiriwa na Trump mwenyewe, siyo watu Obama au watu wa Democrat. Kuna shahidi ambaye alimchangia Trump dola million moja lakini alitoa ushahidi.

Partisanship huwa ipo kila siku, tangu mwaka 1993, ila viongozi wa juu wamekuwa wanaipunguzia sana makali; kwa mfano mwaka 2006 wakati democrats walipochukua madaraka, George Bush alizungumza na Nancy Pelosi kuwa wafanye kazi za nchi kwa kushirikiana vizuri, na wala hakukuwa na vurugu za kupigiana makelele ingawa bado kuna watu (Including Trump mwenyewe) waliuokuwa wanasema Demcrats wam-impeach Bush kwa sababu ya vita ya Iraq. Hata mwaka 2010 wakati Republicans walipochukua Bunge tena, Obama alishirikiana nao tu lakini wao, hasa Eric Canton na Mitch McConnel walikataa kushirikiana na Obama wakisikiliza pia kelele za kuta kum-impeach Obama kuwa hakuzaliwa Marekani (Hata Trump mwenyewe alipiga sana kelele hizi). McConnel akaahidi kuwa atahakikisha Obama atakuwa one term president na hivyo kumwekea vizingitia kwa kila alilofanya ikiwa ni pamoja na kukataa kujaza nafasi nyingi sana za majajai mka jaji wa Mahakama Kuu, na wala Obama hakufanya reciprocity ya namna hiyo. Trump alipochukua madaraka alijenga ukabila wa kutoshirikiana kabisa na Democrats na kuanza kujenga uhasama, ndiye rais wa Kwanza kwa zaidi ya miaka 50 kuwa na cabinet ya kutoka chama kimoja tu. Ingawa kelele za impeach trump zilikuwapo, na zitaendelea kuwapo kwa kila rais atakayefuata, hazikuwa msingi wa impeachment hii ambayo imetokana na ushahidi wa matumizi mabaya ya madaraka, na kuvunja katiba kwa kukikuka Article 1 ya katiba kuhusu Oversight powers za Congress.
 
Pamoja na yote hawambandui Trump. Hata yeye mwenyewe anajua
 
Ni mara chache sana kumkuta mwana CCM mwenye uelewa, uwezo, kujitambua na akili kama wewe. Kwa bahati mbaya na wewe umendeeleza takwimu kuwa real.
 
Wazungu si waonevu kiasi hicho, usiwalinganishe na hawa washabiki maandazi, kama ni kosa ni kosa lipo kama halipo halipo kweli mzungu uchukia uongo na rushwa kuliko kitu chochote duniani.
 
Fikra za namna hii ni hatari sana kwenye Taifa.
Unajua chanzo cha ethinic conflicts duniani kote?

Unafuatilia hata kujua chanzo cha machafuko huko Ethiopia? Hivi kumbe kiporo kina madhara kwenye ubongo kweli.
 
Trump afunguliwa mashtaka kwa kutumia madaraka vibaya na kuzuia uchunguzi


Baraza la Wawakilishi likipiga kura wakati Spika wa Bunge Nancy Pelosi wa California, akiwa mbele yao. Kura hiyo ni kupitisha kifungu cha pili cha kumfungulia mashtaka ya kumuondoa madarakani Rais Donald Trump, Jumatano, Disemba 18, 2019, huko Bungeni, Washington. AP Photo/Patric

Baraza la Wawakilishi Jumatano usiku limemkuta na makosa Rais Donald Trump kwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kujinufaisha yeye mwenyewe na pia kuzuia juhudi za bunge kuchunguza vitendo vyake.

Katika kura ambapo kila upande wa chama uliegemea upande wake, Baraza la Wawakilishi linalodhibitiwa na Wademokrat lilipitisha vifungu viwili vya kumshtaki Trump, Mrepublikan, na hivyo kufanya awe rais wa tatu wa Marekani kufunguliwa mashtaka katika historia ya miaka 243 ya nchi hii.

Trump ambaye amekejeli tuhuma za mashtaka yaliyo funguliwa kumuondoa madarakani na kuwashambulia Wademokrat kwa kushinikiza hilo, hivi sasa kuna uwezekano wakukabiliwa na kesi mwezi Januari 2020, katika Baraza la Seneti.

Lakini Warepublikan waliowengi katika Baraza la Seneti inatarajiwa zaidi kutomuondoa madarakani, na hivyo kuwaachia wapiga kura kuamua juu ya hatma yake Trump wakati akiomba muhula wa pili kurejea White House katika uchaguzi mkuu Novemba inayokuja.
White House imetoa tamko mara tu baada kupigwa kura, inayosema, “Leo ndiyo kilele cha tukio la kuaibisha la kisiasa katika Baraza la Wawakilishi katika historia ya taifa letu. Imesema hatua hiyo ni “mashtaka ya uongo.”

Tamko hilo limeongeza kusema, “Rais anayakini kuwa Baraza la Seneti litarejesha hali ya kawaida, yenye haki, na mchakato wa sheria, vyote hivyo vilipuuziwa katika mjadala wa Baraza la Wawakilishi. Yuko tayari kwa hatua zinazofuata na hana shaka kuwa atakutikana hana makosa kabisa.”

Baraza la Wawakilishi lilijadili faida za kumfungulia Trump mashtaka ya kumuondoa madarakani kwa zaidi ya masaa sita kabla ya kupiga kura. Wawakilishi wa chama cha Demokrat waliendeleza suala la kufunguliwa mashtaka Trump.

Walikinzana na Warepublikan, wanaosema kuwa Trump hakufanya makosa yoyote katika juhudi zake za kushinikiza kwa kipindi cha mwezi mzima Ukraine ichunguze mmoja wa mahasimu wa kisiasa wa Trump wa chama cha Demokrat katika uchaguzi wa mwaka 2020, shughuli za kampuni ya gesi yenye tija ya Makamu wa Rais Joe Biden, mtoto wake Hunter Biden, na nadharia iliyojitokeza kuwa Ukraine iliingilia kati uchaguzi mkuu wa 2016 ambao Trump alishinda, ili kuhujumu kampeni yake.

Trump alimtaka Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amchunguze Biden katika mazungumzo ya simu mwishoni mwa Julai wakati ambapo alikuwa amezuilia kwa muda msaada wa kijeshi uliokuwa umetolewa kwa ajili ya Kyiv wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 391 ambao mji wa Kyiv ulikuwa unataka utumike kusaidia kupambana na waasi wa nchi hiyo waliojitenga wanaosaidiwa na Russia huko Ukraine mashariki
Hatimaye Trump alitoa fedha hizo Septemba bila ya Zelenskiy kuanzisha uchunguzi dhidi ya Biden, hivyo Warepublikan walisema wakati wa majadiliano ndani ya Bunge kuwa ni ushahidi kwamba Trump alikuwa hajajihusisha na kitendo chochote cha kudai kufanyiwa fadhila na Ukraine kumchunguza Biden kama ni malipo ya msaada huo wa kijeshi.

Moja ya vifungu hivyo vya kumfungulia mashtaka kilichopitishwa na Baraza hilo kilimshutumu Trump kwa kutumia vibaya madaraka yake ya urais kwa kuomba fadhila kutoka serikali ya kigeni ya Ukraine, kufanya uchunguzi ili kumsaidia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi dhidi ya Biden, ambaye anaongoza katika kura za maoni za Wademokrat kitaifa katika uchaguzi wa kumtafuta mteule wa urais atakaye pambana na Trump mwaka 2020.

Madai ya shtaka la pili yalisema Trump alizuia maelfu ya nyaraka zinazohusiana na Ukraine kuwasilishwa kwa wachunguzi wa Baraza la Wawakilishi waliokuwa wanamchunguza ili kufungua mshtaka ya kumuondoa madarakani na kisha aliwazuia maafisa muhimu ndani ya uongozi wake kuja kuhojiwa wakati wa wiki za majadiliano yaliyokuwa yanaendeshwa na kamati zilizokua zimedhibitiwa na Wademokrat yakijikita katika vitendo vya Trump vinavyohusiana na Ukraine.
 
Baraza la Wawakilishi Jumatano usiku limemkuta na makosa Rais Donald Trump kwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kujinufaisha yeye mwenyewe na pia kuzuia juhudi za bunge kuchunguza vitendo vyake.
 
So odds are there that Mike Pence is going to be the next President of the USA.
Uwezekano wa hizo odds ni asilimia 0.0005 , Nancy pelosi spika wa house kwa sasa anasua sura kupeleka hii impeachment hata inayofuata ambako ni senate, na endapo wakisusia basi hii kesi itafutwa by default, na hata kama labda itaenda senate trump atafurahi sana maana kule wanachama wake ni asilimia 53 na inahitajika asilimia 67 ya watu wanaopiga kura za ndio ili trump atoke..Narudia tena na nisikike kwa umaskini, uwezekano wa trump kutolewa ni asilimia 0.00005
 
nadhan unajua kinachoendelea sasa kuhusu hio Russian collusion........ soma ripoti ya Durhan! na bado anaendelea na uchunguzi


au hujasikia kwamba team hillary ilifund ile dossier? vipi hujasikia uhuni uliofanyika kwenye appliction ya FISA?.... ok, nadhan umesoma!

btw, hizo media ulizotaja uko serious kweli? hizo ndio credible media source leo? MSM kwa asilimia kubwa wamejitanabaisha kwamba wanapambana na trump..... huwezi kuwategemea walete habari fair..... zimeegemea dems zaidi!

nashauri usome ripoti ya durhan kuhusu origin of RC utaelewa kwanini nakwambia usiziamin sana hizo media ulizotaja,....... kina comey matumbo joto
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marekani wamefungua tena mlango wa kuangamiza mataifa yatakayoiga huu utaratibu..
 
Brother! Humu ndani watu wanakupinga bure tu Ila upo sahihi! Na kilichotokea jana Dems wamepata aibu sana! Dems wamemzushia Trump mazingaombwe kibao wakiambiwa walete ushahidi wanaleta ushahidi wakupikwa ambao mwisho wa siku wanafeli.

Ndiyo maana jana Trump kawaambia hata kama wakimu' impeach atakuwa ni rais wa kwanza kufanyiwa impeachment pasipo kuwa na crime ya aina yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…