Don Gorgon
Member
- Nov 21, 2024
- 35
- 68
Nimetafuta sana press conference ya ACT Wazalendo waliyofanya jana jioni kuhusu ukamatwaji wa Abdul Nondo iliyoongozwa na kiongozi mmoja wa ACT. Nimebahatika kuipata ikiwa imerushwa na ICON TV tu. Labda mtanisaidia kama kuna pahala inapatikana kwa sauti yenye ubora.
Lakini nilichoona ni kipaza sauti kimoja pekee. Na sauti ilikuwa chini mno. Sikuweza kusikiliza hoja za ACT kuhusu jambo walilokuwa wanataka kulieleza kwa Watanzania kuhusu hatma ya Nondo. Kwa tamko la tukio kubwa kama hilo lilipaswa kuwa organized vizuri na ujumbe ukafika.
Je, ACT Wazalendo hawakualika vyombo vingine? Na kama wajibu wa Vyombo vya Habari kutafuta habari na kuwafikishia wananchi, mbona hawakuhudhuria? Maana ACT walitangaza mapema kuwa watakuwa na press conference, na kwa uzito wa jambo lenyewe wanahabari walipaswa kuwepo kusikia kuwa baada ya masaa mengi, chama kina taarifa gani mpya kuhusu Bw. Abdul.
Je, vyombo vingine vilihofia kuhudhuria ile press au ni waandishi ndiyo walihofia kusambaza taarifa ya tukio hilo toka kwa ACT kwa kuhofia kushughulikiwa? Au kwakuwa ni press huenda haikuwa na chochote kitu?
Press yenyewe hii hapa:
View: https://www.youtube.com/live/qrqrB0o3MS4